Back

ⓘ Mdudu Mikia-mitatu
Mdudu Mikia-mitatu
                                     

ⓘ Mdudu Mikia-mitatu

Wadudu mikia-mitatu ni arithropodi wadogo wa oda Thysanura katika nusungeli Apterygota ya ngeli Insecta. Mikia mitatu ya wadudu hawa ni kwa kweli serki ndefu mbili na epiprokti iliyorefuka. Kiwiliwili chao ni bapa chenye umbo la yai au kimerefuka. Vipapasio ni kinamo na vipande vya mdomo ni vifupi na havikubobea. Hawana macho au macho ni madogo tu. Kiunzi-nje cha wadudu hawa si ngumu na kimefunikika kwa vigamba ambavyo vina rangi ya fedha mara nyingi. Kwa sababu ya hiyo na mwendo wao unaofanana na kuogelea, spishi kadhaa huitwa kisamaki-fedha. Kwa kawaida huonekana katika mazingira manyevu, pengine katika mazingira makavu. Visamaki-fedha huishi mara nyingi katika nyumba ambapo hula nafaka, lahamu, karatasi, wanga katika nguo, vitambaa vya rayoni na nyama iliyokauka. Spishi nyingine huishi katika mapango au katika vichuguu.

Users also searched:

...
...
...