Back

ⓘ Aleksanda wa Hales
Aleksanda wa Hales
                                     

ⓘ Aleksanda wa Hales

Aleksanda wa Hales, O.F.M., aliyeitwa Doctor Irrefragibilis, yaani Mwalimu asiyepingika na Theologorum Monarcha alikuwa mwanateolojia na mwanafalsafa maarufu katika kustawisha Teolojia ya shule na Shule ya Kifransisko.

                                     

1. Maisha

Aleksanda alizaliwa katika familia tajiri kidogo huko Hales, Shropshire leo Halesowen, West Midlands, Uingereza, kati ya mwaka 1180 na 1186.

Alisomea chuo kikuu cha Paris akapata digrii ya mwalimu kidogo kabla ya mwaka 1210.

Alianza kufundisha teolojia mwaka 1212 au 1213, akashika uongozi mwaka 1220 au 1221.

Ndiye aliyekifanya kitabu cha Kauli cha Petro Lombardo kuwa cha kiada katika masomo ya teolojia.

Ugomvi ulipotokea chuoni mwaka 1229, Aleksanda akawa mjumbe mmojawapo kwenda Roma kujadili nafasi ya Aristotle katika mtaala.

Baada ya kurudi Uingereza alipopewa vyeo mbalimbali, alirudi kufundisha Paris (1232-1233, halafu akateuliwa katika tume nyingine kwa ajili ya amani kati ya nchi yake asili na Ufaransa.

Mwaka 1236 au 1237, akiwa na umri wa miaka 50 hivi, Aleksanda alishangaza wote kwa kujiunga na Ndugu Wadogo, akawa hivyo Mfransisko wa kwanza kuwa mwalimu wa chuo kikuu. Misimamo yake ikawa misingi ya shule ya Kifransisko katika teolojia.

Aliendelea kufundisha na kuwakilisha chuo kikuu hicho hata katika Mtaguso wa kwanza wa Lyon (1245.

Aliporudi Paris, aliugua akafariki baada ya kumuachia nafasi yake Mfansisko mwingine, Yohane wa La Rochelle.

Kati ya wanafunzi wake wengi, anangaa Bonaventura wa Bagnoregio; ingawa hakuna hakika kama aliwahi kufundishwa naye, alimfanya "baba na mwalimu" wake, akikusudia "kufuata nyayo zake".

                                     

2. Maandishi yake

 • Alexander of Hales. Quaestiones disputatae antequam esset frater. Edited by the Quarracchi Fathers. Bibliotheca Franciscana scholastica medii aevi, t. 19-21. Quaracchi: Collegii S. Bonaventurae,1960.
 • Alexander of Hales. Glossa in quatuor libros sententiarum Petri Lombardi. Edited by the Quaracchi Fathers. Bibliotheca Franciscana scholastica medii aevi, t. 12-15. Rome: Collegii S. Bonaventurae, 1951-1957.
 • Alexander of Hales Attributed. Summa universis theologiae, Summa fratris Alexandri, edited by Bernardini Klumper and the Quarracchi Fathers, 4 vols. Rome: Collegii S. Bonaventurae, 1924-1948.
                                     

3. Marejeo

 • Wood, Rega." Distinct Ideas and Perfect Solicitude: Alexander of Hales, Richard Rufus, and Odo Rigaldus.” Franciscan Studies 53 1993, 8-13.
 • Principe, Walter H. Alexander of Hales’ Theology of the Hypostatic Union. Vol. 2 of The Theology of the Hypostatic Union in the Early Thirteenth Century Toronto: PIMS, 1967.
 • Fornaro, Italo. La teologia dellimmagine nella Glossa di Alessandro di Hales Vicenza, 1985.
 • Cullen, Christopher M." Alexander of Hales,” in Companion to Philosophy in the Middle Ages, edited by Jorge J.E. Gracia and Timothy B. Noone. Oxford: Blackwell, 2006, 104-109.
 • Russell, Frederick H." Just War” in The Cambridge History of Medieval Philosophy, edited by Robert Pasnau and Christina Van Dyke. New York: Cambridge University Press, 2010, 602-603.
 • Colish, Marcia L. Studies in Scolasticism Aldershot: Ashgate, 2006, 132-133.
 • Boehner, Philotheus. The History of the Franciscan School, I. Alexander of Hales; II. John of Rupella – Saint Bonaventure; III. Duns Scotus; Pt. IV. William Ockham, St. Bonaventure, N.Y.: St. Bonaventure University, 1943-1946.
 • Young, Abigail A." Accessus ad Alexandrum: the Prefatio to the Postilla in Iohannis Euangelium of Alexander of Hales 1186?-1245.” Mediaeval Studies 52 1990, 1-23.
 • Coolman, Boyd Taylor." Alexander of Hales,” in The Spiritual Senses: Perceiving God in Western Christianity, edited by Paul L. Gavrilyuk and Sarah Coakley. New York: Cambridge University Press, 2011, 121-139.
 • Peter Lombard. Sententiarum libri quattuor. Edited by the Quaracchi Fathers. Spicilegium Bonaventurianum 4, 5. Grottaferrata: Collegium S. Bonaventurae, 1971-1981. English translation by Giulio Silano, The Sentences. 4 vols. Toronto: PIMS, 2007-2010.
 • Osborne, Kenan B." Alexander of Hales,” in The History of Franciscan Theology edited by idem. St. Bonaventure, NY: Franciscan Institute Publications, 1994.
 • Brady, Ignatius. C." Sacred Scripture in the early franciscan school, in La Sacra Scrittura e i francescani. Studium Biblicum Franciscanum. Rome, 1973, 65-82.
 • Backus, Irena. The Reception of the Church of Fathers in the West: From the Carolingians to the Maurists. Leiden: Brill, 1997, 301-303.
 • Beiting, Christopher. "The Idea of Limbo in Alexander of Hales and Bonaventure” in Franciscan Studies 57 1999, 4-8.