Back

ⓘ Anwani ya kijiografia
Anwani ya kijiografia
                                     

ⓘ Anwani ya kijiografia

Anwani ya kijiografia ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo 90° za kaskazini na 90° za kusini.

Latitudo za kaskazini na kusini kwa ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" =north au kaskazini na "S" south au kusini au kwa alama za "+" kaskazini na "-" kusini.

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich karibu na London, mji mkuu wa Uingereza.

Kwa mfano, anwani ya National Theater mjini Accra Ghana ni: 5°3314"N latitudo na 0°122"W longitudo.

Anwani inaandikwa mara nyingi kwa njia ya desimali pia na hapa inawezekana kutaja mahali kikakilifu zaidi. Hapo majiranukta vya Ikulu jijini Dar es Salaam ni: -6.815592.39.298204.

                                     

1. Matumizi ya anwani ya kijiografia kwenye wikipedia

Wahariri wengi wanaongeza anwani ya kijiografia katika makala zinazohusu miji, kata, majengo au mahali pengine. Katika wikipedia hii tunaweza kutumia kigezo:coord. Inatosha kunakili mfano kutoka ukurasa wa kigezo hiki na kubadilisha tarakimu zilizopo kwa namba zinazopatikana kwa kutumia GeoNames, Google Earth au ramani nyingine inayotuhusu kuona anwani ya kijiografia.

Users also searched:

idadi ya watu mikoa ya tanzania, ramani ya tanzania na barabara kuu,

...
...
...