Back

ⓘ Leo mfiadini
Leo mfiadini
                                     

ⓘ Leo mfiadini

Leo Somma wa Corigliano Calabro alikuwa mmojawapo kati ya wenzi wa Danieli Fasanella waliofia dini huko Ceuta tarehe 10 Oktoba 1227. Walikuwa Ndugu Wadogo wamisionari huko Moroko.Wote walikuwa mapadri isipokuwa Donulus.

Walitangazwa watakatifu na Papa Leo X mwaka 1516.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 10 Oktoba.

                                     

1. Historia

Kifodini cha Berardo wa Carbio na wenzake kilichotokea Moroko mwaka 1219 kilifanya Wafransisko wengi watamani kufuata nyayo zao kwa kuhubiri Injili kwa wasio Wakristo.

Basi, mwaka 1227, uilofuata ule wa kifo cha mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, watawa 6 wa kanda ya Toscana, Agnelus, Samueli, Donulus, Leo mwenyewe, Hugolino na Nikola wa Sassoferrato, walimuomba Elia wa Cortona, mkuu wa shirika, awaruhusu kwenda Moroko kuwahubiria Waislamu.

Kisha kukubaliwa, walikwenda Hispania, alipojiunga nao kama kiongozi Danieli Fasanella wa Belvedere, mkuu wa kanda ya Calabria.

Toka huko walivuka bahari na tarehe 20 Septemba walishukia Afrika, walipobaki siku chache katika kijiji kilichokaliwa hasa na wafanyabiashara Wakristo.

Halafu, Jumapili asubuhi, waliingia mjini Ceuta, wakaanza mara kuhubiri kwa kupinga Uislamu. Kwa sababu hiyo walipekelekwa kwa sultani ambaye, akiwadhani ni vichaa, aliagiza watiwe gerezani. Walibaki humo hadi Jumapili iliyofuata, ambapo sultani kwa mabembelezo na vitisho alijaribu kuwafanya wakane dini yao.

Aliposhindwa, aliagiza wauawe. Kila mmojawao alimkaribia Danieli ili kupata baraka yake na ruhusa ya kumfia Yesu. Wote walikatwa kichwa.

                                     
  • kuwa shemasi, padri akachaguliwa kuwa askofu mwaka 249 na hatimaye akawa mfiadini Yanapatikana katika magombo 3 na 4 ya Patrologia Latina. Kitabu chake
  • wa Wavandali, mfuasi wa Uario. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini Sikukuu yake na ya wenzake huadhimishwa tarehe 22 Mei. Watakatifu wa Agano
  • Machi - Mtakatifu Yohane wa Triora, padre, mmisionari na mfiadini nchini Uchina 22 Agosti - Papa Leo XII 9 Mei - Nikolaus von Zinzendorf, askofu wa Kanisa
  • Orikuli alikuwa Mkristo wa Tunisia ya leo Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Novemba. Watakatifu wa
  • Mkatoliki na mfiadini nchini Uchina 1900 - Mtakatifu Yosefu Maria Gambaro, Mfransisko padri na mmisionari mfiadini nchini Uchina 1968 - Leo Sowerby, mtunzi
  • Mtakatifu Yosefu Yuan Zaide, padri mfiadini wa China Dingiswayo kiongozi wa Wamthethwa katika eneo la Afrika Kusini ya leo anauawa na Wandandwe vitani. Wikimedia
  • Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei. Andeoli alizaliwa Smirna
  • alifariki 483 alikuwa askofu wa mji huo leo nchini Tunisia hadi alipopelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Corsica leo nchini Ufaransa kutokana na dhuluma

Users also searched:

...
...
...