Back

ⓘ Mana
Mana
                                     

ⓘ Mana

Mana ni chakula kilichotumiwa na Waisraeli walipotangatanga katika jangwa la Sinai miaka 40 mfululizo baada ya kutolewa na Musa nchini Misri walipokuwa wananyanyaswa.

Habari hizo zinapatikana katika vitabu vingi vya Biblia hasa Kutoka 16:1-36 na Hesabu 11:1-9 na vilevile katika Kurani 5:27.

Pamoja na maelezo mbalimbali yaliyotolewa na wataalamu kuhusu asili ya chakula hicho, kwa imani kilitazamwa kama ishara ya pekee ya Mungu kuwashughulikia watu wake.

Yesu alikitumia hicho pia kujitambulisha ni nani kwa binadamu wote: "Mimi ndimi chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni" Yoh 6.

                                     

1. Fumbuzi za kisayansi

Wanasayansi wamejaribu kufumbua kitu hicho cha mana. Ufumbuzi mmoja ni kwamba mana ni sandarusi ya mchamwino, mti unaomea sana katika Rasi ya Sinai. Sandarusi hii ni tamu na ikiwa imekauka ina rangi ya hudhurungi.

Ufumbuzi mwingine ni kwamba mana ni mchozo wa wadudu kama vidukari na wadudu-gamba, k.m. mdudu-gamba wa mchamwino Trabutina mannipara. Katika hali ya hewa moto na kavu ya Rasi ya Sinai mchozo huo hukauka haraka. Fuwele za mchozo huo ni tamu na zina rangi ya manjano au hudhurungi. Mara nyingi michozo kama huo huitwa mana pia.

                                     

2. Marejeo

 • Heinrich, Clark 2002. Magic Mushrooms in Religion and Alchemy. Rochester, VT: Park Street Press. ISBN 0-89281-997-9.
 • McKenna, Terence 1993. Food of the Gods: The Search for the Original Tree of Knowledge, A Radical History of Plants, Drugs, and Human Evolution. New York, NY: Bantam Books. ISBN 0-553-37130-4.
 • Merkur, Dan 2000. The Mystery of Manna: The Psychedelic Sacrament of the Bible. Rochester, VT: Park Street Press. ISBN 0-89281-772-0.
 • Arthur, James 2000. Mushrooms and Mankind: The Impact of Mushrooms on Human Consciousness and Religion. Escondido, CA: Book Tree. ISBN 1-58509-151-0.
                                     

3. Viungo vya nje

 • Devotion and Use of the Manna of Saint Nicholas
 • chabad.org, The Manna
 • Catholic Encyclopedia, Manna
 • Jewish Encyclopedia, Manna
 • Lycaeum Archived Novemba 14, 2013 at the Wayback Machine., Manna as a mushroom
                                     
 • Ndiyo Tidak Hapana Siapa nama anda? Jina lako ni nani? Anda berasal dari mana Unatoka wapi? Bisa bahasa Inggris? Unazungumza kiingereza? Terima kasih
 • Double Beat Und Bodys Tovuti www.lordi.fi Wanachama wa sasa Mr. Lordi Amen OX Mana Hella Wanachama wa zamani G - Stealer Magnum Kalma Enary Kita Otus Awa

Users also searched:

...
...
...