Back

ⓘ Blogu
                                               

Azimio la Dodoma

Azimio la Dodoma ni makubaliano ya wanablogu wa Kiswahili wa Tanzania waliokutana jijini Dodoma kuhusu njia za kuendeleza blogu za wanablogu wa Tanzania kwa kuwa na maadili yanayoendana na utu, heshima, na kanuni za uandishi wa habari. Mkutano huo ulifanyika 7 Aprili 2006.

                                               

Global Voices Online

Global Voices ni mradi ulio chini ya Kituo cha Intaneti na Jamii cha Berkman kilicho chini ya Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Harvard. Mradi huu una blogu ambayo kazi yake ni kuandika muhtasari wa masuala yanayoandikwa na kuzungumziwa katika blogu mbalimbali duniani. Waanzilishi wa mradi huu ni Ethan Zuckerman na Rebecca Mackinonn.

                                               

Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania

Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania ni chama cha wanablogu wa Tanzania. Chama hiki kinaongozwa na Ramadhani Msangi, Simon Kitururu na Da Mija. Nia ya Jumuwata ni kusaidia Watanzania kuweza kufaidika na mabadiliko ya teknolojia kama vile blogu, podikasti, n.k.

Users also searched:

...