Back

ⓘ Luxemburg
Luxemburg
                                     

ⓘ Luxemburg

Luxemburg pia: Lasembagi ni nchi ndogo katika Ulaya. Imepakana na Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani.

Ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya, tena ilikuwa kati ya nchi sita zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya mwaka 1957.

                                     

1. Historia

Luxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.

Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Ujerumani.

Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.

Baada ya vita za Napoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna 1815 ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe iliungwa katika Shirikisho la Ujerumani.

Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani 1866 Luxemburg haikujiunga 1870 na Dola jipya la Ujerumani.

Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee 1890.

                                     

2. Watu

Ina wakazi 613.894 Januari 2019 katika eneo la km² 2.586 pekee. Kati yao 49.1% ni wahamiaji kutoka Ureno 18.2% za wakazi wote, Ufaransa 13.5%, Ujerumani 10.3%, Italia 3.4%, Ubelgiji 3.3%, na nchi nyingine.

Lugha ya taifa ni Kiluxemburg ambayo ni lahaja ya Kijerumani yenye athira nyingi za Kifaransa. Karibu wakazi wote huweza kuongea lugha hizo zote tatu na Kiingereza, lakini zaidi Kifaransa.

Upande wa dini, 68.7% ni Wakatoliki na 3.7% ni Wakristo wa madhehebu mengine. Waislamu ni 2.3%. Wasio na dini ni 26.8%.

                                     

3. Marejeo

 • Kreins, Jean-Marie 2003. Histoire du Luxembourg, 3rd in French, Paris: Presses Universitaires de France. ISBN 978-2-13-053852-3.
 • Thewes, Guy July 2003. Les gouvernements du Grand-Duché de Luxembourg depuis 1848 PDF, Édition limitée in French, Luxembourg City: Service Information et Presse. ISBN 2-87999-118-8. Retrieved on 10 July 2007.
                                     

4. Viungo vya nje

 • Luxembourg profile from the BBC News
 • Luxembourg entry at The World Factbook
 • CEE- Europe’s Digital Competitiveness Report –Volume 2: i2010 –ICT Country Profiles- page 40-41 Archived Septemba 25, 2013 at the Wayback Machine.
 • Plan daction national luxembourgeois en matière de TIC et de haut-débit Archived Septemba 25, 2013 at the Wayback Machine.
 • Luxembourgs Constitution of 1868 with Amendments through 2009, English Translation 2012
 • Official website Kifaransa
 • Art and Culture in Luxembourg
 • Wikimedia Atlas of Luxembourg
 • Luxembourg Archived Agosti 29, 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
 • Luxemburg katika Open Directory Project
 • Inauguration of LU-CIX Archived Februari 21, 2011 at the Wayback Machine.
                                     
 • Schifflange ni mji wa Luxemburg katika Wilaya ya Luxembourg. Orodha ya miji ya Luxemburg
 • Pétange ni mji wa Luxemburg katika Wilaya ya Luxembourg. Orodha ya miji ya Luxemburg
 • Esch - sur - Alzette ni mji wa Luxemburg katika Wilaya ya Luxembourg. Orodha ya miji ya Luxemburg
 • Xavier Bettel amezaliwa 3 Machi 1973 ni mwanasiasa wa Luxemburg ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Luxemburg tangu mwaka 2013.
 • nyingi nchi zifuatazo zinazohesabiwa kuwa Ulaya ya Magharibi: Isle of Man Luxemburg Monako Ubelgiji Ueire Ufaransa Uholanzi Ufalme wa Muungano Uingereza
 • Jules Hoffmann amezaliwa 2 Agosti, 1941 ni mwanabiolojia kutoka nchi ya Luxemburg na Ufaransa. Hasa alichunguza kingamwili. Mwaka wa 2011, pamoja na Bruce
 • LU au lu ni kifupi cha: Kodi ya ICAO ya Moldova Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Luxemburg
 • na maeneo yake ya ng ambo Ubelgiji ya Kusini, Uswisi ya Magharibi, Luxemburg na Kanada. Inazungumzwa pia katika nchi nyingi za Afrika kama vile Jamhuri
 • Huzungumzwa hasa katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswisi, Liechtenstein na Luxemburg Kuna pia wasemaji asilia katika nchi jirani za Ujerumani Austria kama
 • 964 965 966 967 Makala hii inahusu mwaka 963 BK Baada ya Kristo Chanzo cha mji wa Luxemburg Wikimedia Commons ina media kuhusu: 963
 • km² 674, 843 na idadi ya wakazi ni 63, 044, 000. Imepakana na Ubelgiji, Luxemburg Ujerumani, Uswisi, Italia, Monako, Andorra na Hispania. Ufaransa ulikuwa

Users also searched:

...
...
...