Back

ⓘ Jongoo
Jongoo
                                     

ⓘ Jongoo

Majongoo ni aina za arithropodi wembamba na warefu katika ngeli Diplopoda ya nusufaila Myriapoda wenye miguu mingi. Wanafanana kijuujuu na tandu lakini hawa huenda mbio na hula wanyama wengine. Majongoo huenda polepole na hula dutu ya viumbehai, viani na kuvu.

Hata kama kwa Kiingereza majongoo huitwa millipedes miguu elfu na tandu huitwa centipedes miguu mia, kwa ukweli wana idadi karibu sawa ya miguu: tandu wana miguu 16 hadi 300 na majongoo 36 hadi 750.

                                     

1. Spishi kadhaa za Afrika

  • Kylindotherium leve, Jongoo-tufe wa Witrivier
  • Phryssonotus brevicapensis, Jongoo-nywele wa Mlima wa Meza
  • Spirostreptus seychellarum, Jongoo Panda wa Shelisheli
  • Sphaerotherium giganteum, Jongoo-tufe Kusi
  • Archispirostreptus gigas, Jongoo Panda Giant African millipede

Users also searched:

...
...
...