Back

ⓘ Mbu
Mbu
                                     

ⓘ Mbu

Mbu ni wadudu wadogo wa nusuoda Nematocera katika oda Diptera. Kwa asili jina hili limetumika kwa wadudu wa familia Culicidae, lakini kwa sababu spishi nyingi za Nematocera hazina majina ya Kiswahili," mbu” linapendekezwa kama jina kwa Nematocera wote. Nusuoda nyingine ya Diptera, Brachycera, inashirikisha nzi na jamaa wao. Spishi ndogo za Nematocera huitwa usubi au visubi.

Diptera wote wana mabawa mawili tu yaliyopo kwa mesotoraksi. Mabawa ya nyuma ya asili yamepunguzika na kubadilika kuwa virungu halteres ambavyo vinasaidia mdudu ajue mkao wake na mabadiliko ya mwelekeo kama aina ya gurudumu tuzi. Vipapasio vya Nematocera ni virefu kiasi na vina mapingili mengi kuliko Brachycera. Madume ya spishi nyingi zinabeba nywele nyingi juu ya vipapasio. Sehemu za kinywa za mbu zimetoholewa kwa kufyunza. Mara nyingi zinaweza kudunga, k.m. katika spishi zinazofyunza damu.

Spishi za mbu zinazojulikana sana ni zile ambazo hufyunza damu. Ni majike ambao wanafyunza damu, kwa sababu lazima wakuze mayai. Madume na spishi nyingine za mbu hufyunza mbochi au utomvu. Mbu waladamu hurithisha magonjwa mara nyingi, k.m. malaria spishi za anofelesi Anopheles), homanyongo, homa ya vipindi, chikungunya spishi za Aedes na matende spishi za kuleksi Culex).

Lava wa spishi nyingi zaidi huishi katika maji ambapo hula viani, bakteria na vijidudu wengine. Lava waambua ngozi mara nne kabla ya kuwa bundo. Akikomaa bundo aelea juu ya maji au apanda juu ya mmea wa maji na mdumili atoka.

                                     

1. Spishi kadhaa za Afrika

  • Anopheles funestus, Anofelesi Kamata
  • Culex quinquefasciatus, Kuleksi Mabaka-matano
  • Culex thalassius, Kuleksi-pwani
  • Anopheles gambiae, Anofelesi wa Gambia
  • Aedes albopictus, Mbu-misitu
  • Aedes aegypti, Mbu wa Homanyongo

Users also searched:

...
...
...