Back

ⓘ Maporomoko ya maji
Maporomoko ya maji
                                     

ⓘ Maporomoko ya maji

Kwa matumizi mengine ya jina angalia maporomoko

Maporomoko ya maji ni mahali ambako maji yanatelemka juu ya kona kwenye mtelemko na kuelekea chini. Kwa kawaida ni sehemu ya njia ya mto au kijito pale ambako maji yanatelemka juu ya ukingo wa mwamba. Lakini inaweza kutokea pia kwenye ukingo wa barafuto pale ambako maji ya myeyuko yanatelemka.

                                     

1. Kutokea na kubadilika kwa maporomoko ya maji

Maporomoko ya maji hutokea kwa kawaida katika sehemu za juu ya njia ya mto. Hapa mtelemko kwa jumla ni mkubwa zaidi na mwendo wa maji haraka zaidi. Kwa hiyo nguvu ya maji ni kubwa zaidi kiasi inaweza kuchimba lalio hadi imekuwa mfereji kama korongo mrefu.

Pale ambako mwendo wa maji ni juu ya mwamba mgumu mmomonyoko hutokea polepole tu. Pale yanapofikia mahali ambako mwamba mgumu wa juu unakwisha nguvu ya maji yakitelemka kwenye ukingo inachimba lalio ya chini. Chini ya ukingo hutokea dimbwi yenye kizingia cha maji. Maji yanayozunguko humo pamoja na mawe na mchanga ndani yake yanasuguana kwenye ukuta wa mwamba. Kwa njia upeno au nusu pango hutokea. Kama kuna mwamba laini chini ya takaba ya mwamba mgumu wa juu upanuzi wa pango unaendelea haraka zaidi. Baada ya muda upeno unakatika na kuanguka.

Kwa njia hii ukingo wa maporomoko unarudi nyuma na kurudisha njia ya korongo nyuma. Kasi ya harakati inategemea na tabia za mwamba unaopatikana. Kuna maporomoko yanayorudi nyuma mita na nusu kila mwaka.

Baada ya muda wa kutosha wakati mwingine miaka mamillioni nguvu ya maji umeondoa mwamba wa kutosha hali hakuna maporomoko tena na ngazi katika njia imekuwa mtelemko tu.

                                     
  • kuna maporomoko makubwa chini ya uso wa bahari ambako maji baridi kutoka Aktiki hushuka zaidi ya mita 3, 000 kuelekea vilindi vya Atlantiki. Maporomoko hayo
  • Mto Kongo yaani inabeba maji mengi kuliko matawimto mengine. Inawezekana pia kusema ni jina la mto Kongo juu ya Maporomoko ya Boyoma karibu na mji wa
  • ya maji inayopitiwa na meli za mtoni. Upande wa Lualaba kuna sehemu kadhaa zinazofaa kwa meli lakini njia ya maji inakatwa mara kadhaa na maporomoko
  • baada ya chanzo, unageuka tena kuelekea mashariki hadi bahari. Km 35 baada ya kuungana na mto Lujenda pana maporomoko ya Upinde. Km 160 kabla ya kufika
  • una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni. Orodha ya milima ya Tanzania
  • taifa ya Udzungwa, kwa kuwa una maporomoko ya maji yenye urefu wa mita zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya ukungu
  • mwa Misri kwenda kusini hadi Jebel Barkal, kwenye maporomoko ya nne, wakati wa kupanuka kwake Karne ya 15 KK Ustaarabu huo ulidumu kwa karibu milenia
  • mahali pa urithi wa dunia. Maajabu ya Pamukkale ni maporomoko ya maji ya moto yenye kiwango kikubwa cha chumvi ya chokaa. Chokaa hiki kiliganda kwa karne
  • Kilimanjaro, milima ya Usambara, milima ya Udzungwa pia mbuga za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Manyara tena maporomoko ya maji ya mto Ruaha

Users also searched:

...
...
...