Back

ⓘ Kikwaya
                                     

ⓘ Kikwaya

Kikwaya ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wakwaya na Waruri katika mashariki ya upwa wa ziwa Nyanza. Mwaka wa 2005 idadi ya wasemaji wa Kikwaya imehesabiwa kuwa watu 115.000, yaani Wakwaya 70.000 na Waruri 45.000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikwaya iko katika kundi la E20.

                                     

1. Lugha au lahaja?

Katika tasnifu yake ya MA 1977 Massamba analinganisha eCi-Ruuri, eCi-Jita na eKi-Kwaaya na anaonesha wazi kwamba kiisimu lugha hizo zinaweza kuhesabika kama lahaja za lugha moja, ingawa kijamii kila lugha inajihesabu kama lugha kwa upeke wake.

                                     

2. Viungo vya nje

 • makala za OLAC kuhusu Kikwaya
 • lugha ya Kikwaya kwenye Multitree
 • lugha ya Kikwaya katika Glottolog
 • tovuti hiyo ina msamiati wa Kikwaya na wa Kiruri
 • Archived Oktoba 4, 2006 at the Wayback Machine.
                                     

3. Marejeo

 • Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. Orientalia et africana gothoburgensia, no 17. Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6

Kitabu hiki kinataja marejeo mengine kama:

 • Massamba, David. 1982. Aspects of accent and tone in Ci-Ruri. PhD thesis. Indiana University at Bloomington. Kurasa 260.
 • Massamba, David P. 1977. A comparative study of the Ruri, Jita and Kwaya" languages” of the eastern shores of Lake Nyanza Victoria. Tasnifu. University of Dar es Salaam. Kurasa iii, 138.
 • Massamba, David. 1984. Tone in Ci-Ruri. Katika: Autosegmental studies in Bantu tone Publications in African languages and linguistics, vol 3, uk.235-254. Kuhaririwa na George N. Clements & John A. Goldsmith. Berlin & Dordrecht: Mouton de Gruyter; Foris Publications.
 • Massamba, David. 2000. Ci-Ruri verbal inflection. Katika: Lugha za Tanzania / Languages of Tanzania: studies dedicated to the memory of Prof. Clement Maganga CNWS publications, no 89, uk.111-126. Kuhaririwa na Kulikoyela K. Kahigi, Yared M. Kihore & Maarten Mous. Leiden: Research School of Asian, African and Amerindian Studies CNWS, Leiden University.


                                     
 • Ziwa Viktoria. Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 102, 000 hivi. Lugha yao ni Kikwaya mojawapo ya lugha za Kibantu katika jamii ya lugha za Kiniger - Kongo. Inaendana
 • Mkoa wa Geita Lugha yao ni Kikara. Lugha hiyo inafanana sana na Kijita na Kikwaya lugha ambazo huzungumzwa na Wajita na Wakwaya makabila ambayo hupatikana
 • Kikimbu Kikinga Kikisankasa Kikisi Kikonongo Kikuria Kikutu Kikw adza Kikwaya Kikwere Kilambya Kilangi Kilogooli Kiluguru Kiluo Kimaasai Kimachame Kimachinga
 • Malcolm Guthrie Kikara iko katika kundi la E20. Inafanana na Kijita 81 na Kikwaya 80 lugha ya Kikara kwenye Multitree makala za OLAC kuhusu Kikara lugha

Users also searched:

...
...
...