Back

ⓘ Mgongo kati wa Atlantiki
Mgongo kati wa Atlantiki
                                     

ⓘ Mgongo kati wa Atlantiki

Mgongo kati wa Atlantiki ni safu ya milima chini ya maji ya bahari ya Atlantiki inayoelekea kutoka 87°N hadi kisiwa cha Bouvet kusini mwa dunia kwenye 54°S.

Vilele vya juu vya milima hiyo vinaonekana juu ya UB kama visiwa. Safu hiyo ya milima imetokea mahali ambako mabamba ya gandunia yanaachana: bamba la Ulaya-Asia na bamba la Amerika ya Kaskazini katika Atlantiki ya Kaskazini, halafu bamba la Amerika ya Kusini na bamba la Afrika katika Atlantiki ya Kusini.

Mabamba hayo yana mwendo wa kuachana na katika nafasi kati yake magma hupanda juu inayokuwa mwamba mpya uliosababisha kutokea kwa milima ya safu.

Kutambuliwa kwa safu hiyo kuliweka msingi kwa nadharia ya upanuzi wa misingi ya bahari unaosababisha mwendo wa mabamba ya gandunia.

                                     

1. Visiwa vya mgongo kati wa Atlantiki

Visiwa ambavyo ni vilele vya milima ya mgongo huo ni kama vifuatavyo katika mabano ni majina ya vilele vya juu na kimo:

Nusudunia ya kaskazini Atlantiki ya Kaskazini

  • Jan Mayen Beerenberg, m 2277
  • Saint Peter and Paul Rocks Southwest Rock, m 22.5
  • Bermuda Town Hill kwenye kisiwa cha Main Island, m 76 Bermuda ilianza juu ya mgongo lakini imesogea mbali sasa
  • Azori Ponta do Pico au Pico Alto kwenye kisiwa cha Pico, m 2.351
  • Iceland Hvannadalshnúkur in the Vatnajökull, m 2.109.6

Nusudunia ya kusini Atlantiki ya Kusini

  • Tristan da Cunha Queen Marys Peak, m 2062
  • Kisiwa cha Bouvet Olavtoppen, m 780
  • Kisiwa cha Gough Edinburgh Peak, m 909
  • Kisiwa cha Ascension

Users also searched:

...
...
...