Back

ⓘ Mchwa
Mchwa
                                     

ⓘ Mchwa

Mchwa ni wadudu wadogo wa oda ya chini Isoptera katika oda Blattodea wanaoishi kwa makoloni makubwa katika vichuguu. Kuna aina ya mchwa ambao huishi ndani ya mbao au miti. Takriban spishi zote hula ubao.

Kila koloni lina malkia, mfalme, askari na wafanyakazi. Askari na wafanyakazi hawana mabawa lakini malkia na mfalme waliwahi kuwa na mabawa walipokuwa vijana. Mfalme anamtia malkia mbegu na huyu anazaa mayai mengi sana. Askari wanalinda kichuguu na wafanyakazi wanafanya kazi nyingine zote.

Mara kwa mara wafanyakazi wanawapatia majana kadhaa chakula fulani ili wawe wadudu wanaoweza kuzaa. Wadudu hawa wana mabawa na huitwa kumbikumbi.

Utafiti wa hivi karibuni waonyesha mchwa, hasa mchwa wa Jangwa la Sahara, kuwa ndiye mnyama anayestahimili joto zaidi. Spishi hii ya mchwa inaweza kustahimili joto hadi nyuzi 55.1.

                                     

1. Bidii na umoja

Mdudu huyu huishi kwa kushirikiana na kutangamana. Yeye halali kabla hajatafuta chakula cha kutosha na cha kuweka akiba.

Hivyo mchwa wametumika katika hadithi nyingi za kitoto ili kufunza maadili ya bidii na umoja. Kwa kawaida, mchwa hukaa wote pamoja katika koloni.

Mwandishi Aesop pia aliandika kuhusu bidii ya mchwa katika hadithi yake The Ant and the Grasshopper.

Katika maandiko ya Biblia kitabu cha Methali, waumini wameombwa waige mchwa katika utendakazi na umoja.

Katika kitabu kitakatifu cha Waislamu cha Kurani, Sulemani alisikia mchwa akiwaonya wengine warudi nyumbani wasije wakapondwapondwa.

                                     

2. Usumbufu wa mchwa

Hata hivyo, watu wengi huona mchwa kama wasumbufu, haswa anapoishi karibu na majengo ya watu. Mchwa hula mbao na kwa hiyo huharibu milango, samani na maboriti ya nyumba.

Wale wanaoishi ndani ya mbao na kula vifaa vya mbao nyumbani huleta pia tatizo la uchafu kutokana na kinyesi chao. Kwa hiyo, watu wengi hutafuta dawa za kuua wadudu hawa au njia nyingine asili za kuwadhibiti kama vile utumizi wa udongo Diatomaceous au mafuta ya kitunguu saumu zinazoathiri wadudu.

Wanaofanya taaluma hiyo kwanza huangalia mchwa ni wa aina gani ili waweze kujua amejificha wapi maana wao hujifinya pahala kwingi.

                                     

3. Spishi kadhaa za Afrika

 • Hodotermes mossambicus, Mchwa Mvunaji
 • Cubitermes ugandensis
 • Macrotermes natalensis
 • Odontotermes tanganicus, Mwcha-meno wa Tanga
 • Microtermes alluaudanus, Mchwa Mdogo wa Aluauda
 • Trinervitermes trinervoides, Mchwa-pua Mvunaji
 • Pseudacanthoterms spiniger, Mchwa Miiba
 • Coptotermes amanii
 • Macrotermes michaelseni, Mchwa Mkubwa wa Michaelsen
                                     

4. Marejeo

 • AntBase – a taxonomic database with literature sources
 • Ant Genera of the World – distribution maps
 • The super-nettles. A dermatologists guide to ants-in-the-plants
 • AntWiki – Bringing Ants to the World
 • Ant Species Fact Sheets from the National Pest Management Association on Argentine, Carpenter, Pharaoh, Odorous, and other ant species
 • AntWeb from The California Academy of Sciences

Users also searched:

...
...
...