Back

ⓘ Maria Magdalena
Maria Magdalena
                                     

ⓘ Maria Magdalena

Maria Magdalena, yaani wa Magdala ni mmoja kati ya wanafunzi maarufu zaidi wa Yesu wa Nazareti, hasa kutokana na sifa ya kuwa wa kwanza kumuona amefufuka.

                                     

1. Habari zake kadiri ya Injili

Ni kwamba, kadiri ya Injili, baada ya kushuhudia kifo cha Yesu na mazishi yake Mk 15:40-16:1; Math 27:56-28:1; Yoh 19:25, upendo na juhudi vilimfanya mwanamke huyo awahi kwenye kaburi lake alfajiri ya siku ya Jumapili. Huko alitokewa na malaika na kuambiwa amefufuka.

Ndiye aliyewapasha habari hiyo mitume wa Yesu kabla hawajaenda kaburini na kulikuta halina maiti.

Baada ya Maria, hao pia walitokewa na Yesu mwenyewe, kuanzia mtume Petro.

Kabla hajaanza kumfuata, Maria alikuwa amepagawa na mapepo saba Mk 16:9. Alipoponywa na Yesu, alijitolea kumhudumia na mali yake pamoja na wanawake wengine Lk 8:2.

                                     

2. Habari yake kuu katika Yoh 20

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, "Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka."

3 Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini.

4 Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini.

5 Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani.

6 Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda,

7 na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake.

8 Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyemtangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaaamini.

9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu).

10 Basi, hao wanafunzi wakarudi nyumbani.

11 Maria alikuwa amesimama nje ya kaburi, akilia. Huku akiwa bado analia, aliinama na kuchungulia kaburini,

12 akawaona malaika wawili waliovaa mavazi meupe, wameketi pale mwili wa Yesu ulipokuwa umelazwa, mmoja kichwani na wa pili miguuni.

13 Hao malaika wakamwuliza, "Mama, kwa nini unalia?" Naye akawaambia, "Wamemwondoa Bwana wangu, na wala sijui walikomweka!"

14 Baada ya kusema hayo, aligeuka nyuma, akamwona Yesu amesimama hapo, lakini asitambue ya kuwa ni Yesu.

15 Yesu akamwuliza, "Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?" Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, "Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua."

16 Yesu akamwambia, "Maria!" Naye Maria akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, "Raboni" yaani "Mwalimu".

17 Yesu akamwambia, "Usinishike; sijakwenda bado juu kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu uwaambie: nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu."

18 Hivyo Maria Magdalene akaenda akawapa habari wale wanafunzi kuwa amemwona Bwana, na kwamba alikuwa amemwambia hivyo.

                                     

3. Heshima aliyopewa baada ya kufa

Maria Magdalena anahesabiwa mtakatifu katika madhehebu mengi ya Ukristo, akiadhimishwa tarehe 22 Julai. Katika Kanisa la Kilatini Papa Fransisko ameipa hadhi ya sikukuu.

                                     

4. Marejeo

 • Shoemaker, Stephen J. "Rethinking the Gnostic Mary’: Mary of Nazareth and Mary of Magdala in Early Christian Tradition." in Journal of Early Christian Studies, 9 2001 pp 555–595.
 • Wellborn, Amy. De-coding Mary Magdalene: Truth, Legend, and Lies. Huntington, Indiana: Our Sunday Visitor, 2006. ISBN 1-59276-209-3. A straightforward accounting of what is well-known of Mary Magdalene.
 • Burstein, Dan, and Arne J. De Keijzer. Secrets of Mary Magdalene. New York: CDS Books, 2006. ISBN 1-59315-205-1.
 • Acocella, Joan. "The Saintly Sinner: The Two-Thousand-Year Obsession with Mary Magdalene." The New Yorker, 13 and 20 Februari 2006, p. 140–49. Prompted by controversy surrounding Dan Browns The Da Vinci Code.
 • Kripal, Jeffrey John. 2007, The Serpents Gift: Gnostic Reflections on the Study of Religion, Chicago: The University of Chicago Press, ISBN 0226453804 ISBN 0-226-45381-2.
 • Jansen, Katherine Ludwig. The Making of the Magdalen: Preaching and Popular Devotion in the Later Middle Ages. Princeton, N.J.: Princeton University Press, 2000. ISBN 0-691-05850-4.
 • Pearson, Birger A. "Did Jesus Marry?." Bible Review, Spring 2005, pp 32–39 & 47. Discussion of complete texts.
 • Picknett, Lynn, and Clive Prince. The Templar Revelation. New York: Simon & Schuster, 1997. ISBN 0-593-03870-3. Presents a hypothesis that Mary Magdalene was a priestess who was Jesus partner in a sacred marriage.
 • Thiering, Barbara. Jesus the Man: Decoding the Real Story of Jesus and Mary Magdalene. New York: Simon & Schulster Atria Books, 2006. ISBN 1-4165-4138-1.
 • Brock, Ann Graham. Mary Magdalene, The First Apostle: The Struggle for Authority. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press, 2003. ISBN 0-674-00966-5. Discusses issues of apostolic authority in the gospels and the Gospel of Peter the competition between Peter and Mary, especially in chapter 7, "The Replacement of Mary Magdalene: A Strategy for Eliminating the Competition."


                                     

5. Viungo vya nje

 • The Life of St. Mary Magdalene: Saint of the Christian Church Archived Mei 6, 2015 at the Wayback Machine.
 • Miriam/Myriam MGadola: Mary Magdalene
 • "Saint Mary Magdalene." Encyclopædia Britannica Online.
 • The Pesher Technique: The Marriage of Jesus by Barbara Thiering
 • Early Christian Writings: Gospel of Mary
 • Convent of Saint Mary Magdalene
 • St Mary Magdalene, Catholic Encyclopaedia 1911
 • Showing inaccuracy of The Da Vinci Code in respect to Mary Magdalene
 • "St. Mary Magdalen", Butlers Lives of the Saints
 • St Mary Magdalen and the case for the ordination of women in the Catholic Church Archived Machi 2, 2007 at the Wayback Machine.
 • Legends of Mary Magdalene
 • Articles and more than 40 Paintings
 • Gospel of Mary Magdalene
                                     
 • Magdalena Miaka miwili baadaye aliingia shirika la Mabinti wa Maria wa Reunion na tarehe 15 Mei 1877 aliweka nadhiri za kitawa akaitwa Sista Maria
 • Septemba, lakini ya kwake na ya wenzake watano Petro Hong Pyongju, Maria Yi Indok, Magdalena Son So - byg, Agata Yi Kyng - i, Agata Kwon Chin - i ni tarehe 31 Januari
 • lakini ya kwake na ya wenzake watano Augustino Pak Chongwon, Maria Yi Indok, Magdalena Son So - byg, Agata Yi Kyng - i, Agata Kwn Chin - i ni tarehe 31 Januari
 • ya wenzake watano Augustino Pak Chongwon, Petro Hong Pyongju, Maria Yi Indok, Magdalena Son So - byg, Agata Kwn Chin - i ni tarehe 31 Januari. Mwishoni mwa
 • ya wenzake watano Augustino Pak Chongwon, Petro Hong Pyongju, Maria Yi Indok, Magdalena Son So - byg, Agata Yi Kyng - i ni tarehe 31 Januari. Mwishoni mwa
 • tarehe 3 Aprili 1965 huko San Juan, Pwetoriko. Alizikwa katika Santa Maria Magdalena de Pazzis katika eneo la Old San Juan. Orodha ya waandishi wa Pwetoriko
 • aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka Lk 24: 5 - 6 Halafu Maria Magdalena Petro na Mitume wenzake, hata watu zaidi ya mia tano walimuona na
 • na kuanzishwa jumuia mpya. Kufuatana na mifano ya Yesu Kristo na Bikira Maria Agano Jipya linatoa habari za wanaume na wanawake waliojinyima ndoa kwa

Users also searched:

...
...
...