Back

ⓘ Agnes wa Praha
Agnes wa Praha
                                     

ⓘ Agnes wa Praha

Agnes wa Praha alizaliwa Praha mwaka 1211 akafariki huko tarehe 2 Machi 1282).

Mwanzilishi na abesi wa monasteri ya Mt. Fransisko mjini Praha, alianzisha pia Shirika la Wanamsalaba wa Nyota Nyekundu.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira, hasa katika tarehe ya kifo chake au tarehe 6 Machi.

                                     

1. Maisha

Binti wa mfalme wa Bohemia Ottokar I na Kostanza wa Hungaria, alikuwa ndugu wa jirani wa watakatifu Ludmila, Venseslaus, Edwiga, Elizabeti wa Hungaria na Margerita wa Hungaria.

Kisha kulelewa katika monasteri ya masista wa Citeaux huko Trzebnica, na ya masista wa Premontree huko Doksany, alipokuwa na miaka 8 alitumwa kwenye ikulu ya Vienna ili kuandaliwa awe mke wa kaisari Henri VII wa Ujerumani, mwana wa Federiko II.

Akiguswa na mfano wa Fransisko wa Asizi, aliamua kuishi kitawa na kwa msaada wa Papa Gregori IX alivunja uchumba wake akarudi Praha.

Huko alianzisha konventi ya kwanza ya Ndugu Wadogo katika eneo hilo1232, ikiwa pamoja na hospitali kwa mafukara: ili kuendesha hospitali hiyo alianzisha chama cha kitume cha Wanamsalaba ambao mwaka 1237 walikubaliwa na Papa kuwa shirika la kitawa.

Mwaka 1234 alianzisha monasteri ya Waklara iliyopokea masista watano waliotumwa na Klara wa Asizi mwenyewe: Agnes alihamia huko tarehe 11 Juni mwaka huohuo. Baadaye akawa abesi wake hadi kifo.

                                     

2. Heshima baada ya kifo

Agnes aliheshimiwa sana mara baada ya kufa: tarehe 28 Novemba 1874 Papa Pius IX alithibitisha heshima hiyo na jina alilopewa la mwenye heri. Tarehe 12 Novemba 1989 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu.

                                     

3. Marejeo kwa Kiswahili

  • Barua zote nne za Klara wa Asizi kwa Agnes wa Praha zinapatikana katika kitabu: MTAKATIFU KLARA WA ASIZI – Maandishi yake – tafsiri ya Ndugu Wafransisko Wakapuchini – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1994 – ISBN 9976-63-414-5
                                     

4. Marejeo mengine

  • Seton, Walter W. Some New Sources for the Life of Blessed Agnes of Bohemia: Including a Fourteenth-Century Latin Version. Cambridge: Cambridge University Press 2010. ISBN 1108017606
                                     

5. Viungo vya nje

  • Article at Catholic Encyclopedia
  • Czechs Dedicate Year to Saint Who Felled Communism Archived Septemba 27, 2012 at the Wayback Machine.
  • Vatican page on Agnes of Bohemias canonization Kiitalia
  • Monastery of Saint Agnes of Bohemia, Prague

Users also searched:

...
...
...