Back

ⓘ Abushiri ibn Salim al-Harthi
Abushiri ibn Salim al-Harthi
                                     

ⓘ Abushiri ibn Salim al-Harthi

Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya Pangani na pwani ya Tanzania ya leo mnamo 1889.

Alikuwa mfanyabiashara na mwenye mashamba ya miwa karibu na Pangani.

Mnamo Agosti 1889 aliongoza upinzani dhidi ya utawala wa Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki katika eneo la Pangani.

Baada ya miezi ya mapambano taz. vita ya Abushiri alikamatwa na hatimaye kunyongwa na Wajerumani tarehe 16 Desemba 1889.

                                     

1. Marejeo

  • Pugu hadi Peramiho - kimehaririwa na P. Gerold Rupper, OSB, BPNP, Peramiho 1988, ISBN 9967 67 031 1
  • Glassmann, J.: Bushiri bin Salim, makala katika Dictionary of African Biography, ed. Emmanuel Kwaku Akyeampong & Steven J. Niven, uk. 13f, ISBN-13: 978-0195382075, ISBN-10: 0195382072

Users also searched:

...
...
...