Back

ⓘ Age Aint Nothing But a Number
Age Aint Nothing But a Number
                                     

ⓘ Age Aint Nothing But a Number

Age Aint Nothing but a Number ni jina la kutaja albamu ya kwanza ya msanii wa rekodi za muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, Aaliyah. Albamu ilitolewa chini ya studio ya Jive na Blackground Records mnamo tar. 13 Juni 1994, huko nchini Marekani. Baada ya kuingia mkataba na mjombake Barry Hankerson, Aaliyah akatambulishwa kwa msanii na mtayarishaji wa rekodi R. Kelly. Akawa mshauri na mtu wake wa karibu, vilevile akiwa kama mtunzi na mtayarishaji mkuu wa albamu hii.

Wawili hao wamerekodi albamu katika Chicago Recording Company huko mjini Chicago, Illinois. Albamu imetoa vibao vikali viwili, ikiwa ni pamoja na kupata chati katika kumi bora kwa kibao cha "Back & Forth" na "At Your Best You Are Love"; single zote mbili zilitunukiwa Dhahabu na Recording Industry Association of America RIAA. Single mbili za ziadi zilifuata: "Age Aint Nothing But a Number" na "No One Knows How to Love Me Quite Like You Do".

Age Aint Nothing But a Number imepokea tahakiki za kiupendeleo na haki kutoka kwa watalaamu wa uhakiki. Albamu iliingia nafasi ya 18 kwenye chati za Billboard 200 na kuuza nakala milioni tatu kwa nchini Marekani, ambapo ilipata kutunukiwa platinamu mara mbili na RIAA mnao tar. 24 Oktoba 2001.

                                     

1. Orodha ya nyimbo

Nyimbo zote zimetungwa na R. Kelly, kasoro zile zilizowekewa maelezo.

 • "Down with the Clique" – 3:24
 • "Street Thing" – 4:58
 • "Im Down" – 3:16
 • "Intro" – 1:30
 • "The Thing I Like" UK bonus track – 3:23
 • "No One Knows How to Love Me Quite Like You Do" – 4:07
 • "Back & Forth" – 3:51
 • "Back & Forth Mr. Lee & R. Kellys Remix" bonus track – 3:43
 • "Old School" – 3:17
 • "Young Nation" – 4:41
 • "Im So into You" – 3:26
 • "Throw Your Hands Up" – 3:34
 • "At Your Best You Are Love" – 4:52
 • "Age Aint Nothing But a Number" – 4:14
                                     

2. Marejeo

 • Farley, John 2002. Aaliyah: More Than a Woman. Simon & Schuster. ISBN 0743455665.
 • Sutherland, William 2005. Aaliyah Remembered. Trafford Publishing. ISBN 1412050626.
 • Brackett, Nathan; Hoard, Christian David 2004. The New Rolling Stone Album Guide: Completely Revised and Updated 4th Edition. Simon & Schuster. ISBN 0743201698.
 • Kenyatta, Kelly 2002. An R&B Princess in Words and Pictures. Amber Books Publishing. ISBN 0970222432.

Users also searched:

...
...
...