Back

ⓘ Mafuta ya petroli
Mafuta ya petroli
                                     

ⓘ Mafuta ya petroli

Mafuta ya petroli ni kiowevu kizito chenye rangi nyeusi hadi ya kijani. Inatokea kiasili katika ardhi na inawaka rahisi.

Ni chanzo cha petroli, fueli mbalimbali, dawa nyingi na plastiki: hivyo ni kati ya vyanzo muhimu kabisa vya nishati vinavyotumiwa na binadamu kama fueli ya usafiri na ya kutengeneza umeme.

Kikemia mafuta ya petroli ni mchanganyiko wa dutu, hasa hidrokaboni mbalimbali. Inatumiwa kwa njia ya ukenekaji distillation ikipashwa moto na sehemu zake kutenganishwa zikifikia kiwango cha kuchemka kwa nyakati mbalimbali.

                                     

1. Chanzo cha mafuta ya petroli

Petroliamu hupatikana ndani ya maganda ya mwamba. Wataalamu wengi hukubaliana ya kwamba iliundwa baharini. Maji ya bahari yamejaa algae na planktoni inayoishi kutokana na uwezo wake wa usanisinuru. Viumbehai hao wadogo wanakufa na kuzama chini katika vilindi vya bahari vikifunika tako la bahari kama ganda. Katika kina kirefu cha mita elfu kadhaa mabaki yale hayawezi kuoza kutokana na uhaba wa oksijeni, hivyo yanageuka kuwa ganda la matope.

Kila baada ya muda mashapo mineralia kama vile mchanga, vumbi ya hewani yanashuka pia hadi tako la bahari na kufunika matope yaliyotokea na planktoni. Maganda yale ya mashapo mineralia yanaweza kuwa manene na mazito hadi yakaanza kukandamiza tope na kuisababisha kuwa moto. Katika mazingira ya shindikizo na joto molekuli ndefu za hidrati kabonia za biomasi zinavunjwa kuwa molekuli fupi katika mchakato unaoigwa na teknolojia ya mvevusho.

Molekuli hizo fupi zinatembea katika vinyweleo ndani ya mwamba ya mashapo hadi kufikia aina ya mwamba penye nafasi ndogondogo ambako molekuli nzito zakusanya kama petroliamu na molekuli nyepesi sana kama gesi asilia. Kama kuna ganda la mwamba imara lililopo juu ya mwamba vinyweleo akiba ya petroliamu na gesi inaanza kutokea na mara nyingi molekuli nyepesi za gesi huwa kama "kofia" ya gesi asilia juu ya "ziwa" la petroliamu. Hii ni sababu ya kwamba mara nyingi gesi asilia inapatikana pamoja na petroliamu.

                                     

2. Historia ya matumizi yake

Tangu nyakati za kale mafuta ya petroli ilitokea kiasili kutoka ardhi katika nchi kama Mesopotamia kusini. Pale ilipoonekana kama ziwa iliunganika na oksijeni ya hewa na kuganda kuwa lami. Ile lami asilia iliwahi kutumiwa na watu wa kale; kwa kuikoroga na mchanga watu waliweza kuziba mapengo kati ya Mbao za jahazi.

Pia wenyeji wa Babeli walimwaga tayari mafuta ya petroli asilia juu ya barabara za udongo kwa shauri la kuimarisha uso wake.

Baadaye Waroma wa Kale na Wabizanti walitumia mafuta hayo kama silaha za kumwaga moto dhidi ya maadui hasa baharini.

Lami na mafuta ya petroli zilitumiwa pia kama tiba ya maradhi mbalimbali.

Wakati wa karne ya 19 daktari Mkanada Abraham Gesner aligundua ya kwamba aliweza kutengeneza mafuta ya taa kutoka kwa mafuta hayo. Hadi wakati ule ni hasa mafuta ya nyangumi yaliyotumiwa kama mafuta ya taa lakini ilizidi kuwa ghali. Mafuta mpya yalipokelewa haraka, yalipatikana kwa bei nafuu na katika nchi nyingi watu walianza kutafuta chemchemi asilia za mafuta ya petroli.

Mwishoni mwa karne ya 19 Carl Benz alibuni motokaa iliyotumia injini ya mwako wa ndani kwa kutumia petroli. Kutokana na juhudi za Henry Ford za kujenga motokaa kwa bei ndogo mahitaji ya petroli yaliongezeka tena.

Usambazaji wa motokaa ulisababisha kuzalishwa kwa petroli kwa wingi na haja ya kukwa na mafuta ya petroli kuongezeka.

                                     

3. Uzalishaji wa petroliamu

Jedwali linalofuata linaorodhesha nchi ambako petroliamu hutolewa ardhini kufuatana na wingi wa uzalishaji.

Kipimo cha wingi ni kiasi kinachohesabiwa kwa "mapipa" kwa siku kwa Kiingereza: "barrels per day" - kifupi "bbl/d") ambako "pipa" moja linalingana na lita 159. Hali halisi mapipa hayatumiwi tena na mafuta husafirishwa kwa njia ya bomba.

Chanzo: U.S. Energy Information Administration Archived Julai 10, 2008 at the Wayback Machine.

1 Uzallishaji wa mafuta umeshapita kilele chake katika nchi hii kutokana na jumla ya akiba zake.

2 Uzalishaji kutokana na akiba za kawaida unapungua katika Kanada, lakini uzalishaji kutokana na mchanga mwenye mafuta unaongezeka; pamoja na mafuta yaliyopo ndani ya mchanga akiba za Kanada ni kubwa dunani baada ya Saudia.

3 Iraki ni mwanachama wa OPEC lakini uzalishaji wake haukuhesabiwa katika takwimu za OPEC tangu 1998.

                                     

4. Petroliamu na siasa

Mafuta ya petroli yalijulikana tangu karne nyingi yakawa na matumizi mbalimbali. Tangu mapinduzi ya viwandani umuhimu wake uliongezeka kama mafuta ya kutia grisi kwenye injini pia kama mafuta ya taa katika miji iliyokua haraka. Baada ya kupatikana kwa injini ya mwako wa ndani umuhimu wake uliongezeka tena. Mwingereza Winston Churchill alitangulia kuhakikisha utawala wa kampuni ya Kiingereza juu ya maeneo ya mafuta katika Uajemi kusini mnamo mwaka 1911. Tangu Vita kuu ya kwanza ya Dunia wanasiasa wengine wengi walielewa umuhimu wake wa kijeshi na kiuchumi kwa jumla.

Lakini mafuta ya petroli yanapatikana katika nchi kadhaa tu, tena si kila mahali kwa viwango vikubwa. Hivyo kulitokea mashindano baina ya nchi kubwa namna za kutawala upatikanaji wa mafuta yale. Rais Coolidge wa Marekani alisema mwaka 1924 "kipaumbele cha mataifa kitaonekana kwa utawala wao juu ya mafuta ya petroli na bidhaa zinazotengenezwa kutokana nayo"

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia maazimo mbalimbali yalitawaliwa na shabaha za kukamata au kutetea maeneo yenye petroliamu. Nchi za jangwa za Waarabu kwenye Ghuba la Uajemi kama Saudia, Kuwait na Falme za Kiarabu zenye wakazi wachache zilikuwa maskini lakini tangu upatikanaji wa petroliamu zimekuwa tajiri. Wakati uleule zilipaswa kukubali uhusiano wa karibu sana na Uingereza na baadaye hasa na Marekani uliofanana wakati mwingine na usimamizi.

Wakati wa Vita ya Yom Kippur kwenye mwaka 1973 nchi za Waarabu walitumia mafuta ya petroli kama silaha wakasababisha mgogoro wa bei ya mafuta walipokataa kwa miezi kadhaa kuuza mafuta kwa nchi zilizosaidia Israel vitani, hasa Marekani na nchi za Ulaya Magharibi. Mgogoro huo ulisababisha matatizo ya kiuchumi kote duniani.                                     

5. Matatizo ya matumizi ya petroliamu

Petroliamu ni fueli yenye faida nyingi; inatolewa ardhini kwa urahisi, inasafirishwa haraka na kuwa na nafasi nyingi za kuitumia kwa manufaa ya binadamu. Ilikuwa fueli iliyowezesha maendeleo ya kiuchumi ya karne ya 20.

Siki hizi kuna wasiwasi mwingi kuhusu matumizi yake kama fueli kwa sababu ni fueli kisukuu maana ikitumiwa haiongezeki tena wala kurudi; ilionekana ya kwamba akiba zake zitaishia siku moja. Hapa wasiwasi mkubwa ni ya kwamba uchumi wa dunia umejengwa juu ya msingi unaoendelea kufifia na kuna hatari ya kwamba uchumi utapata mshtuko mkubwa kama akiba za mafuta ya petroli zitaendelea kupungua na bei zake kupanda.

Vilevile matumizi yake yanatoa gesi nyingi hewani amabazo zinaleta hasara kwa mazingira, hasa gesi ya dioksidi kabonia inayochangia kupanda kwa joto duniani kwenye hatari nyingi.

Hapo ndipo sababu kuu za utafiti mwingi kugundua vyanzo vya nishati mbadala.

                                     

6. Viungo vya nje

 • Oil, petroleum: Development, production, consumption and reserves Archived Novemba 16, 2007 at the Wayback Machine.
 • PetroTalk Portal for petro related Articles, Discussion, Links and more
 • Environmental effects of oil extraction Archived Septemba 26, 2009 at the Wayback Machine.
 • US Energy Information Administration - Part of the informative website of the US Governments Energy Information Administration.
 • BP Statistical Review of World Energy
 • World oil consumption World oil consumption

Takwimu

 • European Brent prices Archived Mei 18, 2010 at the Wayback Machine. since 1987
 • Department of Energy EIA - World supply and consumption
 • US petroleum prices Archived Mei 24, 2010 at the Wayback Machine. - from US Department of Energy EIA
 • Department of Energy EIA - Crude Oil and Total Petroleum Imports to USA
                                     
 • Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini. Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi, hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara - Bogas
 • ni nchi ya visiwa na ufalme mdogo katika Ghuba ya Uajemi karibu na pwani ya Saudi Arabia. Nchi ni tajiri kutokana na mapato ya mafuta ya petroli Bahrain
 • moto ya kawaida katika nyumba pasipo na vifaa vikubwa vya umeme. Haifai kwa moto ya vifaa vya umeme au petroli na mafuta Moto za petroli mafuta na aina
 • Paracelsus visivyo na wakazi lakini vina dalili za kuwa na maliasili kama mafuta ya petroli Visiwa hivyi vyote vina pia umuhimu wa kijeshi na kisaisa kwa sababu
 • kuu ya pili ya dunia. Leo hii kuna wakazi zaidi ya 1, 200, 000. Nyumba zote za Dubai ni mpya. Kukua kwa Dubai kulitokana na mapato ya mafuta ya petroli Lakini
 • hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu. Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli yalimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko
 • kwa sababu ni mlango wa kuingia na kutoka Ghuba ya Uajemi penye asili ya sehmu kubwa ya mafuta ya petroli duniani. Ghuba imepakana na Uajemi, Falme za Kiarabu
 • na mlima Dena m 4, 359 Eneo la Zagros ni sehemu muhimu ya uzalishaji wa mafuta ya petroli Zagros, Picha kutoka Iran, Livius Major Peaks of the Zagros
 • mto Mebridege na Noqui kando la Matadi kwenye mpaka wa Kongo. Uchumi ni hasa kilimo na uvuwi pamoja na migodi, kuchimba madini na mafuta ya petroli

Users also searched:

bei ya petrol leo 2021,

...
...
...