Back

ⓘ Maximilian Kolbe
Maximilian Kolbe
                                     

ⓘ Maximilian Kolbe

Maximilian Maria Kolbe alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka nchi ya Poland.

Katika historia ya Kanisa anajulikana kwa jinsi allivyomheshimu Bikira Maria kwa jina la Imakulata, yaani Mkingiwa dhambi asili.

Baada ya kuanzisha chama cha Mashujaa wa Imakulata huko Roma Italia na Mji wa Imakulata huko Polandi, alikwenda Japani kama mmisionari.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alifungwa na wafuasi wa Unazi katika kambi ya wafungwa wa siasa kule Auschwitz. Hatimaye alijitolea kushika nafasi ya mfungwa mwenzake aliyechaguliwa kuachwa bila ya chakula hadi kufa pamoja na wengine 9. Aliwaandaa hao wote kukabili kifo kwa tumaini la Kikristo na bila ya chuki, na alipobaki peke yake aliuawa kwa sindano ya sumu.

Mwaka 1982 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 14 Agosti kila mwaka.

                                     

1. Sala yake

Wewe umenipenda milele, tangu u Mungu; hivyo umenipenda na utanipenda milele!.

Upendo wako kwangu ulikuwepo hata kabla sijakuwepo, na ni kwa sababu ya kunipenda, Mungu mwema, kwamba umeniita kutoka utovu wa vyote nianze kuwepo!

                                     

2. Marejeo

 • B. HANLEY, O.F.M., Maximilian Kolbe, Upendo uliokithiri – tafsiri ya Parokia la Mt. Maksimilian Kolbe, Mwenge, Dar-es-Salaam – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1992
 • Rees, Laurence. Auschwitz: A New History, Public Affairs, 2005. ISBN 1-58648-357-9
                                     

3. Viungo vya nje

 • Kolbes Gift, a play by David Gooderson about Kolbe and his self-sacrifice in Auschwitz based on factual evidence and conversations with the late Józef Garliński
 • Saint Maximilian Kolbe, a popular biography at Catholicism.org
 • Patron Saints Index: Saint Maximilian Kolbe Archived Aprili 16, 2008 at the Wayback Machine.
                                     
 • padri kutoka Hispania na mfiadini nchini Japani 1941 - Mtakatifu Maximilian Kolbe O.F.M.Conv., padri mfiadini kutoka Poland 1941 - Paul Sabatier, mshindi
 • Kristo Buganda inatangazwa kuwa nchi lindwa na Uingereza 8 Januari - Maximilian Kolbe padre mtakatifu kutoka Poland 17 Machi - Paul Green, mwandishi wa
 • mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1954 1894 - Mtakatifu Maximilian Kolbe O.F.M.Conv., padre mfiadini kutoka Poland 1917 - Peter Taylor, mwandishi
 • shirika hilo ni Yosefu wa Kopertino, Fransisko Antonio Fasani na Maximilian Maria Kolbe Siku hizi idadi yao ni 4, 500 hivi duniani kote. Ordo Fratrum Minorum
 • Wikimedia Commons ina media kuhusu: Masalia The First - class Relics of St. Maximilian Kolbe Relics in the Church of St Charles Borromeo, Wrocław, Poland World
 • Tagore, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi, mwaka wa 1913 14 Agosti - Maximilian Kolbe padre mtakatifu kutoka Poland 14 Agosti - Paul Sabatier, mshindi wa

Users also searched:

...
...
...