Back

ⓘ Lalibela, Ethiopia
Lalibela, Ethiopia
                                     

ⓘ Lalibela, Ethiopia

Lalibela ni mji unaopatikana kaskazini mwa Ethiopia. Ni mmoja kati ya miji mitakatifu nchini humo.

Mji huu ni wa pili kwa utakatifu ukifuatia ule wa Aksum, na pia ni patakatifu kwa ajili ya kufanyia hija kwa wakazi wengi wa nchini Ethiopia.

Tofauti na mji wa Aksum, watu wengi katika mji wa Lalibela kwa ujumla ni Wakristo Waorthodoksi wa Mashariki. Lalibela ilikusudiwa kuwa Yerusalemu mpya kama matokeo ya mji wa Yerusalemu kuchukuliwa na Waislamu. Hata majina kadhaa katika kanisa la Lalibela yametokana na majengo mbalimbali katika mji wa Yerusalemu.

Likiwa linapatikana katika ukanda wa Semien Wollo Semien Wollo Zone wa kabila la Amhara au Kilil mita 2.500 juu ya usawa wa bahari.

Kutokana na takwimu za serikali, mwaka 2005, mji wa Lalibela ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao 14.668 ambao kati yao, 7.049 ni wanaume na 7.619 ni wanawake.

Katika Lalibela pia kunapatikana uwanja wa ndege wa Lalibela unaoitwa Lalibela Airport Kodi ya ICAO HALL, IATA LLI, soko kubwa, shule na hospitali moja.

                                     

1. Historia

Katika kipindi cha uongozi cha Mtakatifu Gebre Mesqel Lalibela aliyekuwa wa nasaba ya Zangwe, iliyoongoza kuanzia karne ya 12 hadi karne ya 13 mji wa sasa wa Lalibela ulikuwa ukijulikana kama Roha. Mfalme huyo mtakatifu aliupa mji huo jina hilo kutokana na mambo yaliyotokea wakati wa kuzaliwa kwake, ambayo ndiyo yaliyomfanya mama yake kujua mambo yatakayotokea katika maisha yake ya baadaye kama mfalme wa Ethiopia Negus.

Majina ya sehemu mbalimbali katika mji wa Lalibela yanatokana na majina mbalimbali ambayo Mfalme huyo aliyapata alipokwenda katika mji wa Yerusalemu ambao ni mji mtakatifu Holly Land alipokuwa kijana. Lalibela anaonekana kuuona mji wa Yerusalame na kujaribu kujenga Yerusalemu Mpya kutokana na mji mkongwe wa Yerusalemu kuchukuliwa na Waislamu mwaka 1187.

Kutokana na hali hiyo, mambo mengi ya asili katika mji huo yanatokana na majina ya Biblia, hata jina la mji wenyewe unaojulikana kama Mto Yordani. Ulibaki kuwa mji mkuu wa Ethiopia tangu karne ya 12 na karne ya 13.

Mtu wa kwanza kutoka katika bara la Uropa kufika katika kanisa hili, alikuwa mpelelezi wa Ureno aliyeitwa Pêro da Covilhã 1460 – 1526. Padri wa Kireno aliyeitwa Francisco Álvares 1465 - 1540, alikuwa amesindikizwa na balozi wa Ureno wakati alipotembelea Lebna Dengel mwaka 1520. Katika maelezo yake kuhusiana na miundo aliatamka kwamba," Nachoka kuandika zaidi juu ya haya majengo, kwa sababu inaonekana kwangu kuwa sitaaminika kama nitaongea zaidi… Naapa kwa Mungu, ambaye ni kwa nguvu zake kwamba mimi nipo, kuwa kila nilichokiandika ni ukweli”.

Japokuwa Ramuso alijumuisha mipango ya makanisa mengine ya aina hii katika kitabu chake cha Alvares, haijajulikana bado, ni nani aliyempa hiyo michoro. Mtu mwingine aliyeripotiwa kutembelea Lalibela alikuwa Miguel de Castanhoso, aliyekuwa mwanajeshi chini ya Christovão da Gama na kuondoka katika nchi ya Ethiopia mwaka 1544. Baada ya Castanhoso, zaidi ya miaka 300 ilipita hadi Mzungu mwingine, Gerhard Rohlfs, alipotembelea tena Lalibela muda fulani kati ya miaka 1865 na 1870.

Kwa mujibu wa Futuh al-Habasa wa Sihab ad-Din Ahmad, Ahmad Gragn alichoma moja ya makanisa ya Lalibela katika uvamizi wake nchini Ethiopia.

                                     

2. Makanisa

Eneo hili la kijiji linajulikana duniani kwa makanisa mbalimbali kama vile "kanisa la mwamba mmoja" ambalo linakuwa moja ya sehemu muhimu katika historia ya teknolojia ya ukataji miamba. Tarehe halisi ya kuanzishwa kwa makanisa hayo, haijarekodiwa vizuri, lakini wengi wanajua kuwa yamejengwa katika kipindi cha uongozi wa Lalibela, hasa karne ya 12 na karne ya 13. Makanisa hayo yameorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

Kuna makanisa yapatayo 13, ambayo yapo pamoja katika makundi manne:

Kundi la Makanisa ya upande wa kaskazini: Bete Medhane Alem ambapo ni nyumbani kwa Msalaba wa Lalibela ambalo ndilo linaloaminika kuwa kubwa kuliko yote ya namna hiyo duniani, pengine nakili ya lile la Mtakatifu Maria wa Zion St. Mary of Zion la Aksum. Limeungana na kanisa la Bete Maryam pengine kanisa kongwe kuliko yote. Bete Golgotha linalojulikana kama lenye Kaburi la Mfalme wa Lalibela kanisa dogo la Selassie na kaburi la Adam.

Kundi la Makanisa ya Magharibi: kanisa la Mtakatifu George, Bete Giyorgis, linasemekana kuwa ndilo kanisa linaloongoza kwa michoro mizuri na ndilo kanisa lilituzwa vizuri zaidi.

Kundi la Makanisa ya Mashariki: ni pamoja na kanisa la Bete amanuel pengine ndilo kanisa la kwanza la kifalme na pia linawezekana kuwa gereza la kwanza Bete Abba Libanos na Bete Gabriel-Rufael pengine nyumba ya kwanza ya kifalme linalohusishwa na utakatifu bakery.

Zaidi eneo lililopo katika monasteri ya Ashetan Maryan na kanisa la Yimrehane Kristos ilijengwa kama kumbukumbu ya mume wake baada ya kifo chake.

Tofauti na nadharia zilizoanzishwa na waandishi kama vile Graham Hancock mwamba mkubwa uliotokea na kuwa kanisa la Lalibela haukujengwa kwa msaada wa mfalme Knights Templar: ushahidi mbalimbali umekuwa ukipatikana na kuonesha kuwa, kanisa hilo lilijengwa na watu wa kwanza kuwahi kuishi katika nchi ya Ethiopia.

Kama vile Buxton aliandika kuwa, lilivuta kuja kwa wageni wengi, kujenga kanisa hili na kuongeza kuwa, kuna kila dalili kuwa katika baadhi ya michoro, hutoa muungano na makanisa mengine kama vile makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki ya Ethiopia na Kanisa la Kiorthodoksi la Misri), bado ana wasiwasi kuhusu asili halisi ya miundo hiyo, lakini wazo la hakika linabaki kuwa makanisa haya ya mawe yalifuata makanisa ya kale ambayo yenyewe bado yana mfumo na ushahidi wa mfumo wa asili ya Axum

Makanisa haya bado yanatoa uhandisi wa ajabu, kuwa yana uhusiano na maji ambayo yanapatikana katika chemchemi karibu na makanisa ya aina hiyo na kukaribia kufanana na mfumo wa sayansi ya miamba ya artesians ambayo huleta maji juu ya milima ambapo ndipo mjii hupatikana.

                                     

3. Fasihi

Lalibela inatajwa kuwa mji wa mapadri wengi, makanisa ya miamba katika riwaya ya Tananarive Due, riwaya inayuhusisha udhanifu wa kisansi. My Soul to Keep.

Hancock, Graham, Carol Beckwith & Angela Fisher: African Ark - Peoples of the Horn, Chapter I: Prayers of Stone/The Christian Highlands: Lalibela and Axum, Harvill, An Imprint of HarperCollinsPublishers, ISBN 0-00-272780-3

                                     

4. Soma zaidi

 • David W. Phillipson, Ancient Churches of Ethiopia New Haven: Yale University Press, 2009. Chapter 5, "Lalibela: Eastern Complex and Beta Giyorgis"; Chapter 6, "Lalibela: Northern Complex and Conclusions"
                                     

5. Viungo vya nje

 • History of Lalibela churches Archived Desemba 13, 2004 at the Wayback Machine.
 • Lalibela site page in the Aluka digital library
 • Lalibela, a city carved from legend
 • UNESCO World Heritage Site
 • www.imperialethiopia.org/history2.htm Archived Februari 5, 2004 at the Wayback Machine.
 • Ethiopian Treasures - Zagwe Dynasty, Rock-hewn Churches - Lalibela Archived Septemba 25, 2008 at the Wayback Machine.
 • Ethiopia - Timkat Celebration in Lalibela
                                     
 • Segud Airport Jinka - Baco Airport Kabri Dar - Kabri Dar Airport Lalibela - Lalibela Airport Makale - Alula Aba Nega Airport Shilavo - Shilavo Airport
 • Zammadu Maryam nayo yanakisiwa huenda yalijengwa karne ya 15 Makanisa ya Lalibela yapo katika sehemu za chini za milima. Sehemu ya Uhifadhi wa mlima huu
 • Orodha ya hapo chini inataja watawala wa Ethiopia tangu nasaba ya Zagwe. Wafalme wa Aksum na wafalme wa D mt hawaorodheshwi kutokana na mapengo mengi
 • Bonde la Awash. 1978 - Utamaduni - Makanisa yaliyochongwa mwambani, Lalibela 1979 - Utamaduni - Fasil Ghebbi. 1978 - Asili - Hifadhi ya Taifa ya Semien
 • na Ethiopia kupitia maeneo ya nchi za Waislamu ilikuwa jambo la kubahatisha. Mwaka 1493 mjumbe wa mfalme wa Ureno alifika katika mji mkuu wa Lalibela karibu

Users also searched:

...
...
...