Back

ⓘ Pasifiki
Pasifiki
                                     

ⓘ Pasifiki

Pasifiki ni bahari kubwa kuliko zote duniani.

Pasifiki iko kati ya Bara la Amerika upande wa mashariki na Bara la Asia / Australia upande wa magharibi.

Eneo lake ni kilometa za mraba milioni 179.7 ambayo si bahari kubwa tu bali pia ni eneo kubwa kuliko nchi kavu yote duniani: ni karibu nusu ya uso wa dunia.

Kuna visiwa zaidi ya 25.000 katika Pasifiki; vingi ni vidogo sana. Visiwa hivyo huhesabiwa mara nyingi pamoja na Australia kama "Australia na Pasifiki".

Pasifiki kina cha wastani wa mita 4.028; kina kirefu katika mfereji wa Mariana kinafikia mita 11.034.

Bahari za pembeni ziko hasa upande wa Asia / Australia. Kati ya hizo ni: Bahari ya Celebes, Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China.

Jina la Pasifiki kwa Kilatini: yenye amani, yaani kimya limetokana na Wazungu wa kwanza waliovuka bahari hii mwaka 1520 BK kutoka Amerika ya Kusini hadi Ufilipino wakaikuta kuwa ni bahari tulivu. ù

Lakini Pasifiki inaweza kuwa na dhoruba kali sana. Ni eneo lenye matetemeko ya ardhi mengi yanayosababisha mawimbi haribifu ya tsunami ambayo yalimaliza miji na vijiji ufukoni.

Users also searched:

...
...
...