Back

ⓘ Mali
Mali
                                     

ⓘ Mali

Kwa maana nyingine ya neno hili angalia Mali maana

Mali kwa Kifaransa: République du Mali = Jamhuri ya Mali ni nchi ya Afrika ya Magharibi.

Imepakana na Algeria, Mauretania, Niger, Burkina Faso, Cote dIvoire na Senegal. Mali. Haina pwani kwenye bahari yoyote.

Sehemu ya juu ni mlima wa Hombori Tondo mita 1155 juu ya UB ulioko katikati ya nchi.

Kaskazini sehemu kubwa ya eneo la Mali ni jangwa la Sahara.

Wakazi walio wengi huishi kusini, karibu na mito Senegal na Niger.

                                     

1. Jiografia

Theluthi mbili za eneo la Niger ni jangwa. Maeneo mengine ni ya Sahel na kanda la Sudan. Sehemu za kusini ni hasa tambarare za bonde la mto Niger.

Hali ya hewa ni tofautitofauti, kulingana na eneo. Kuna kanda tatu:

 • Kanda la Sudan lina usimbishaji wa mm 1400. Lina savana ilhali miti inaongezeka hadi kufika hali ya misitu kabisa kusini.
 • Kanda la jangwani kaskazini - usimbishaji chini ya mm 100 kwa mwaka, yabisi na yabisi sana. Hapa wanaishi wafugaji pekee.
 • Kanda la Sahel: mbuga nusu yabisi inayobadilika kuwa savana kusini kwenye mvua zaidi. Kuna kilimo kando ya mto Niger.

Kuna malighafi kama vile dhahabu, urani, fosfati, kaolini, chumvi na chokaa.

                                     

2. Historia

Mali ina historia ndefu ambayo ni historia ya pamoja ya nchi za kanda la Sahel na kanda la Sudan.

Zamani za Wafinisia na za Waroma palikuwa na mawasiliano ya biashara na nchi za Mediteranea kupitia wanafayabiashara Waberberi walioelewa njia za Sahara.

Uvamizi wa Wavandali katika Afrika ya Kaskazini ulivuruga mawasiliano hayo.

Baada ya uvamizi wa Waarabu na uenezaji wa Uislamu biashara ilianza upya. Ndio Waberberi Waislamu walioingiza dini mpya hata kusini ya Sahara.

Katika eneo la Mali ya leo pamoja na nchi jirani ni hasa madola matatu makubwa yaliyotawala upande wa kusini wa njia za biashara iliyovuka Sahara.

                                     

2.1. Historia Dola la Ghana

Dola la kwanza lilikuwa Dola la Ghana. Kuanzia karne ya 8 BK hadi mwaka 1076 lilitawala biashara ya dhahabu, pembe za ndovu na chumvi. Mji mkuu ulikuwa Kumbi Sale wenye wakazi 30.000 katika Mauretania ya leo.

Taarifa za wanahistoria Waarabu zimeonyesha ufalme tajiri. Utamaduni wake haukuwa wa Kiislamu bali wa Kiafrika asilia.

Mwisho wake ulianza wakati jeshi la Wamurabitun kutoka Moroko lilivuka jangwa na kuvamia Kumbi Sale.

                                     

2.2. Historia Milki ya Mali

Milki ya Mali ilianza kama ufalme mdogo wa Wamalinke kando ya Ghana. Wakati wa karne ya 13 ilianza kupanuka chini ya mfalme Sundiata Keita. Sundiata mwenyewe alipokea Uislamu mnamo 1240 BK na wafalme baada yake waliendela kuwa Waislamu.

Mfalme wa Mali aliyejulikana zaidi ndiye Mansa Kankan Musa I 1312–1337. Miaka 1324-1325 alihiji kwenda Makka. Alisafiri na dhahabu nyingi sana. Huku Misri alitoa zawadi kiasi cha kuharibu thamani ya dhahabu kwa miaka 12 iliyofuata.

Wakati ule mji wa Timbuktu ulikuwa kitovu cha biashara na elimu iliyojulikana kote katika umma wa Kiislamu hata Ulaya.

Katika karne ya 14 BK uwezo na utawala wa Mali ulipungua na Songhai ilichukua nafasi yake.

                                     

2.3. Historia Dola la Songhai

Asili ya Wasonghai ilikuwa Nigeria ya Kaskazini ya leo. Walipanua utawala wao kuelekea magharibi wakapokea Uislamu wakati wa uvamizi wa Almurabitun.

Mnamo mwaka 1250 walikuwa chini ya Mali lakini katika karne ya 14 walijipatia uhuru tena, wakaanza kushika maeneo ya Mali yenyewe.

Kilele cha nguvu yake ilikuwa wakati wa mfalme Askia Mohammad I katika karne ya 16 walipotawala eneo kubwa kutoka Kano Nigeria hadi pwani ya Atlantiki. Wakati wake mji wa Timbuktu ilitembelewa na msafiri Leo Africanus aliyeleta baadaye habari za nchi hadi Ulaya.

Utawala wao uliporomoka baada ya mashumbulizi kutoka Moroko mwaka 1591. Wakati ule mataifa ya Ulaya yameshaanza kufika kwenye mwambao wa Afrika ya Magharibi wakifungua biashara ya moja kwa moja na Ulaya. Umuhimu wa biashara ya kuvuka Sahara ulipungua vikali pamoja na faida iliyopatikana kwa watawala katika maeneo ya Sahel.

                                     

2.4. Historia Kipindi cha madola madogo na jihadi

Kilichofuata kilikuwa kipindi cha madola madogo. Viongozi Waislamu walijaribu mara kadhaa kujenga utawala juu ya eneo lote.

Anayejulikana zaidi alikuwa Alhaj Omar aliyepiga vita kwa jina la dini ya Kiislamu dhidi ya Wabambara waliofuata utamaduni na dini asilia za Kiafrika.

Mtoto wa Alhaj Omar aliyeitwa Ahmadu alijaribu kuendeleza jihadi yake. Lakini wakati ule Wafaransa walianza kuenea katika Afrika ya Magharibi wakamshinda.

Mali ikawa koloni la Ufaransa kuanzia mwaka 1895. Ilikuwa sehemu ya Afrika ya Magharibi ya Kifaransa, na kuanzia 1920 ya Sudan ya Kifaransa.

                                     

2.5. Historia Uhuru

Mwaka 1960 Mali pamoja na Senegal zilipata uhuru kama "Shirikisho la Mali". Baada ya Senegal kuacha umoja huo, Jamhuri ya Mali chini ya rais wa kwanza Modibo Keïta ikawa nchi ya kujitegemea.

Keita alipinduliwa mwaka 1968 na wanajeshi akishtakiwa kuwa ameharibu uchumi na kujitajirisha. Kiongozi mpya Moussa Traoré alitawala kama dikteta wa kijeshi, baadaye kwa msaada wa katiba ya chama kimoja.

Mabadiliko yaliyotokea kote Afrika tangu mwisho wa Ukomunisti kuanzia miaka ya 1990 yalisababisha kupinduliwa kwa Traoré katika Machi 1991 na kamati ya kijeshi iliyoongozwa na Amadou Toumani Touré.

Katiba mpya ya mwaka 1992 iliunda kipindi cha kura huru alimoshinda Amadou.

                                     

3. Watu

Katika maeneo makubwa ya kaskazini wanaishi makabila ya Waberberi, hasa Mauri na Watuareg ambao ni wahamaji. Ndio 10% ya wakazi wa nchi wakikalia asilimia kubwa za eneo.

Kikundi kikubwa ndio Wabamana 30% katika eneo la mji mkuu Bamako, halafu wako Wamandinka, Wafula, Wadogon, Wasonghai na wengineo.

Lugha

Kutokana na ukoloni, Kifaransa kimekuwa lugha rasmi. Kibambara kinaeleweka na takriban 60% za wakazi. Kwa ujumla kuna lugha 56 nchini Mali.

Dini

Uislamu ni dini kubwa nchini 90 % za wakazi. Wakristo wanafikia 5% Wakatoliki 3.3% na Waprotestanti 1.7%. Wengine wanafuata dini asilia za Kiafrika 5%.

Ibada na desturi asilia zinapatikana pia katika mazingira ya Waislamu.

                                     

4. Tazama pia

 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
 • Demografia ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
 • Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
                                     

5. Marejeo

 • Constitution of Mali French. A student-translated English version Archived Septemba 12, 2012 at the Wayback Machine. is also available.
 • Milet, Eric and Manaud, Jean-Luc 2007. Mali in French. Editions Olizane. ISBN 2-88086-351-1.
 • Velton, Ross 2004. Mali. Bradt Travel Guides. ISBN 1-84162-077-7.
 • DiPiazza, Francesca Davis 2006. Mali in Pictures. Minneapolis, Minnesota: Learner Publishing Group. ISBN 978-0-8225-6591-8.
 • Mali country profile. Library of Congress Federal Research Division January 2005. This article incorporates text from this source, which is in the public domain.
                                     

6. Viungo vya nje

 • War at the background of Europe: The crisis of Mali
 • Mali Archived Juni 7, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
 • Mali profile from the BBC News
 • Mali 2012 Trade Summary Statistics
 • Kifaransa Serikali ya Mali tovuti rasmi
 • The European Union mission in Mali - Hungarys involvement in the mission
 • Mali katika Open Directory Project
 • Wikimedia Atlas of Mali
 • Mali entry at The World Factbook
 • Kifaransa Secrétariat Général du Gouvernement Malienne Archived Februari 22, 2016 at the Wayback Machine.
                                     
 • mtawala tajiri wa Mali ya Magharibi. Ufalme wa Mali ulikuwa na eneo la zamani la Ufalme wa Ghana kusini mwa Mauritania na Melle Mali na maeneo yaliyo
 • nchi nyingi za Afrika kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Mali Shelisheli, Chad, n.k., Asia ya Kusini na Amerika zilizokuwa makoloni ya
 • kiasi tofauti eneo la Senegal lilikuwa sehemu ya Dola la Ghana, ya Dola la Mali na hatimaye ya Dola la Songhai Baadaye lilikuwa koloni la Ufaransa hadi mwaka
 • hisa huhimiza ugavi wa wenye mali kutoka kwa wanaosimamia utumizi wa mali kwa sababu sio kila wakati watu walio na mali huwa na fikira nzuri ya kibiashara
 • Rais wa Mali anayeshika madaraka tangu mwaka 2013. Alikuwa Waziri Mkuu wa Mali kutoka mwaka 1994 hadi 2000 na Rais wa Bunge la Kitaifa la Mali kutoka 2002
 • mrefu la Bafing. Mto Senegal wenyewe unaanza karibu na mji wa Bafoulabe Mali kwenye maungano ya mito miwili ya Bafing na Bakoye ambayo yote ina chanzo
 • Ingawa kimsingi ni suala la uchumi, unahusika sana na maadili, kwa kuwa mali zinaweza kutumika vizuri au vibaya, hasa upande wa haki za watu wengine
 • maana ya kununua mali ile ikiwa kuna anayekodisha. Huenda mpangaji anataka kumwachia mwenye mali kazi za kurekebisha na kukarabati mali ile na kwa hiyo
 • fomu ya kitu au mipaka yake ya nje, muhtasari, au uso wa nje, kinyume na mali nyingine kama rangi, texture, au muundo wa nyenzo. Wanasaikolojia wameelezea

Users also searched:

loss reports,

...
...
...