Back

ⓘ Madagaska
Madagaska
                                     

ⓘ Madagaska

Kisiwa chenyewe ni cha nne kwa ukubwa duniani.

Upekee wa kisiwa unatokana na kwamba kilimeguka kutoka India miaka milioni 88 hivi iliyopita, halafu kilibaki bila watu hadi karne ya 5 hivi BK.

                                     

1. Ekolojia

Kisiwa hicho ni pia mazingira makubwa ya aina ya violezo ambayo ni asilimia 5 ya violezo vyote vya mimea na wanyama vya dunia nzima.

Asilimia 90 ya viumbehai asili ni maalumu wa Madagaska, kama vile wanyama aina ya kima awali wanaoitwa lemuri, ndege ambao waambukiza ugonjwa na mti wa mbuyu.

                                     

2. Historia

Madagaska ni kati ya maeneo ya mwisho kufikiwa na kukaliwa na binadamu.

Wa kwanza kufika walitokea visiwa vya Indonesia kama mwaka 350-550 BK.

Baadaye tu walihamia watu kutoka bara la Afrika mwaka 1000 hivi na wengineo.

Kuanzia mwaka 1787 hadi mwaka 1897 kisiwa kilizidi kuunganishwa kisiasa chini ya Ufalme wa Merina.

Watawala walikuwa watu kutoka familia ya Andrianampoinimerina, mwanzilishi wa taifa hilo, ambaye alikuwa ametokea katika kabila la Wamerina

Kabila hilo lilikuwa kubwa na muhimu kuliko yote 18 ya kisiwa hicho. Makazi yake yalikuwa katika uwanda wa juu wa kati lakini lilienea sehemu kubwa ya Bukini.

Wamerina walikuwa na makao makuu ya utawala wao Antananarivo; baada ya kugawiwa kwa ufalme wao mnamo 1710 kitovu cha malaka kati ya Wamerina ikahamia kwenye mlima wa Ambohimanga lakini tangu kuunganishwa kwa Wamerina mnamo 1794 mji mkuu ukulikuwa tena Atananarivo. Kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho.

Makabila yote ya wenyeji yalizungumza lugha moja na yalikuwa na mila na desturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujenga umoja wa kiutamaduni uliowafanya wawe jamii moja kimsingi.

Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwa wageni kutoka Uingereza na Ufaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofisha mamlaka ya kifalme.

Kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwa koloni la Ufaransa. Hii ni kwa kuwa, ingawa sera ya kuisasisha ya Bukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wa nchi hiyo wa kutetea uhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofisha ufalme huo kwa kuongeza utegemezi wake kwa mataifa ya kigeni.

                                     

3. Watu

Mwaka 2018 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa milioni 26.3. Wenyeji wengi wana mchanganyiko wa damu: DNA inaonyesha kuwa wakazi wa kwanza kutoka Indonesia wameichangia asilimia 50 hivi na Waafrika vilevile. Wanaoishi sehemu za ndani ni wa Kiindonesia zaidi, wakati wale wa pwani ni wa Kiafrika zaidi.

Lugha

Lugha ya taifa ni Kimalagasi. Lugha rasmi za Madagaska ni Kimalagasi na Kifaransa angalia pia orodha ya lugha za Madagaska.

Dini

Mwaka 1993 nchini Madagaska kulikuwa na dini za jadi 52% hivi, Ukristo 41%, Waprotestanti wakiwazidi kidogo Wakatoliki, Uislamu 7% hivi n.k. Tangu hapo wafuasi wengi wa dini za jadi wameongokea Ukristo, hasa wa Kiprotestanti.

Utamaduni

Pamoja na kutokea mazingira tofauti sana, Wamalagasi wamechanganyikana sana na kuwa na utamaduni na lugha aina moja, ya Kiindonesia zaidi.

                                     

4. Tazama pia

 • Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
 • Demografia ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
                                     

5. Viungo vya nje

 • Country Profile from BBC News
 • Madagascar entry at The World Factbook
 • Madagaska katika Open Directory Project
 • Madagascar Archived Agosti 29, 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
 • Key Development Forecasts for Madagascar from International Futures
 • Wikimedia Atlas of Madagascar

Majiranukta kwenye ramani: 20°S 47°E

                                     
 • Atsimo - Atsinanana ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 621, 200. Mji mkuu ni Farafangana. Wikimedia Commons
 • Vatovavy - Fitovinany ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 1, 097, 700. Mji mkuu ni Manakara. Wikimedia Commons
 • Sofia ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 940, 800. Mji mkuu ni Antsohihy. Msitu wa Anjajavy Wikimedia Commons
 • Boeny ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 543, 200. Mji mkuu ni Mahajanga. Mahajanga Hifadhi ya Taifa ya Namoroka
 • Alaotra - Mangoro ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 877, 700. Mji mkuu ni Ambatondrazaka. Wikimedia Commons
 • Amoron i Mania ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 693, 200. Mji mkuu ni Ambositra. Ambositra Wikimedia Commons
 • Vakinankaratra ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 1, 589, 800. Mji mkuu ni Antsirabe. Antsirabe Belazao Ziwa
 • Anosy ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 544, 200. Mji mkuu ni Tôlanaro. Tôlanaro Hifadhi ya Taifa ya Andohahela
 • Atsimo - Andrefana ni moja ya mikoa 22 ya kujitawala ya Madagaska Idadi ya wakazi wake ni takriban 1, 018, 500. Mji mkuu ni Toliara. Toliara Ifaty Msitu

Users also searched:

...
...
...