Back

ⓘ Koleta Boylet
Koleta Boylet
                                     

ⓘ Koleta Boylet

Nicolette Boylet alizaliwa Corbie tarehe 13 Januari 1381 katika familia duni.

Ni maarufu kwa kuanzisha urekebisho wa matawi mbalimbali ya Wafransisko ambao walioufuata wanaitwa kwa heshima yake Wakoleta.

Kisha kuishi utawani sehemu mbalimbali, akichukia ulegevu uliotawala huko, alijifungia upwekeni 1402-1406, halafu akakubaliwa na antipapa Benedikto XIII ruhusa ya kurekebisha na kuanzisha monasteri ili zifuate ufukara walioutaka Fransisko wa Asizi na Klara wa Asizi.

Alifariki tarehe 6 Machi 1447 huko Gand leo Ubelgiji, katika moja ya monasteri 17 za Waklara alizozianzisha.

Alitangazwa na Papa Klementi XII kuwa mwenye heri tarehe 23 Januari 1740, halafu Papa Pius VII alimtaja kuwa mtakatifu tarehe 24 Mei 1807.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Machi.

                                     
  • Mtakatifu Rosa wa Viterbo, bikira Mfransisko kutoka Italia 1447 - Mtakatifu Koleta Boylet bikira Mfransisko kutoka Ufaransa 1900 - Gottlieb Daimler, mhandisi
  • kanuni 1538 Kwa ajili hiyo mwanzilishi aliikamilisha katiba ya Mt. Koleta Boylet kwa kutumia ile ya Wakapuchini. Sifa ya monasteri ikaenea haraka na
  • bikira 1282 6 Machi Kinga wa Hungaria, bikira 1292 24 Julai Koleta Boylet bikira 1447 6 Machi Katerina wa Bologna, bikira 1463 9 Machi

Users also searched:

...