Back

ⓘ Krismasi
                                               

Christine Fellows

Amezaliwa Windsor, Ontario na kukulia Ufaransa na Kelowna, British Kolumbia. Fellows aliishi Toronto, Vancouver, Gulph na Montreal kabla ya kuhamia Winnipeg mwaka 1992. Mnamo 1992, aliunda kikundi chake cha kwanza, Helen, pamoja na Barry Mirochnick, Paul James, na Chang. Helen alijiengua mwaka 1995, na mwaka 1996 Fellows alijiunga na mwimbaji - mwandishi wa nyimbo Keri McTighe. Barry Mirochnick, Keith McLeod Peggy Messing, kuunda Special Fancy. Kundi lilitoa albamu moja, King Me. Mnamo 2000 Fellows alitoa albamu yake ya kwanza, 2 Little Birds. Hii ilifuatiwa na The Last One Standing mwaka ...

Krismasi
                                     

ⓘ Krismasi

Krismasi ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

                                     

1. Jina

Kuna majina mawili yaliyo kawaida kwa Kiswahili kwa ajili ya sikukuu hii:

 • Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo.
 • Noeli inatokana na neno la Kiingereza "Noel" au "Nowell" ambalo limepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "Noel". Hilo ni ufupisho wa neno la Kilatini "Natalis dies", "siku ya kuzaliwa".
                                     

2. Historia ya sherehe ya Krismasi

Hakuna uhakika ni lini Krismasi ilianza kusheherekewa. Ni sikukuu ya kale katika Ukristo lakini haikuwepo tangu mwanzoni. Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa sababu utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

Lakini baadaye Ukristo ulienea katika Dola la Roma kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi.

Tangu mwanzo wa karne ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

Habari za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana kutoka Misri mnamo mwaka 200 BK. Mwandishi Mkristo Klemens wa Alexandria alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.

Lakini kadirio la tarehe 25 Desemba lina asili katika Misri pia. Kuanzia mwaka 200 kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.

Inaonekana tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.

                                     

3. Krismasi na sikukuu ya Sol Invictus

Mjini Roma wakati wa karne ya 4 tarehe ya Krismasi katika Desemba ilitokea pamoja na sikukuu ya Kipagani iliyoitwa "Siku ya Sol Invictus". Hii ilikuwa sherehe ya Jua kama mungu "Sol invictus" yaani "Jua lisiloshindika". Hii ilikuwa ibada iliyoingia Roma kutoka Uajemi ambako mungu Mithra aliabudiwa kama mungu wa nuru.

Waumini wa dini ya Jua waliona wakati wa Desemba kama kipindi cha pekee kutokana na solistasi ya mwezi huo; katika nusutufe ya kaskazini ya Dunia urefu wa mchana unapungua na usiku unakuwa mrefu tangu sikusare ya 21/22 Septemba hadi tarehe 21/22 Desemba; kuanzia siku za 21/22 Desemba mchana huwa mrefu na nuru inaongezeka. Mwendo huo ulitazamwa kama ushindi wa nuru = Jua juu ya giza.

Pale Roma Kaisari Eliogabalus aliyezaliwa Syria, alitawala Roma 218 hadi 222 alianzisha sherehe ya sikukuu ya "Kuzaliwa Jua" huko Roma. Baadaye Kaisari Aurelianus akaithibitisha rasmi mwaka 273.

Wakati wa Kaisari Licinius 308-324 sikukuu hiyo ilikuwa ikiadhimishwa bado tarehe 19 Desemba. Hatimaye ikahamishiwa tarehe 25 Desemba.

Wataalamu mbalimbali walidai kwamba Kanisa lilipachika sikukuu ya Kristo kwenye tarehe hiyo kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya jua kama mungu "Sol invictus" yaani "Jua lisiloshindika". Kwa namna yoyote hata katika Ukristo Jua linatazamwa kama ishara ya Kristo; katika sehemu mbalimbali za Biblia Kristo alifananishwa tayari na Jua na maneno haya yaliandikwa muda mrefu kabla ya kutokea kwa siku ya Sol Invictus. Mifano ni Injili ya Luka 1.78 Ufunuo 21, 23, Malaki 4.2. Kati ya Waorthodoksi kuna tarehe nyingine, hasa 6 Januari kutokana na tofauti katika kalenda.                                     

4. Habari za Krismasi katika Biblia

Habari za Krismasi kama sherehe hazipatikani katika Biblia kwa sababu zilizotajwa hapa juu na kwa sababu mwanzoni mwa Kanisa mkazo ulikuwa juu ya kifo na ufufuko wa Yesu, tunavyoona hasa katika barua za Mtume Paulo.

Baadaye tu, Wakristo walichunguza zaidi asili ya huyo aliyesadikiwa nao kuwa alikufa na kufufuka.

Hasa vitabu viwili vya Agano Jipya vina habari za kuzaliwa kwake Yesu, yaani Injili za Mathayo na Luka.

                                     

4.1. Habari za Krismasi katika Biblia Katika Injili ya Mathayo

Mathayo anasimulia habari hizo katika mlango wa kwanza kuanzia aya 18 na katika mlango wa pili.

Bikira Maria, Mama wa Yesu, alipata mimba wakati alipokuwa mchumba wa Yosefu. Yosefu alitaka kumwacha lakini aliambiwa na malaika aanze kuishi naye na kumkubali mtoto kama wake kwa kumpa jina "Yesu".

Mamajusi kutoka mashariki waliwatembelea kijijini Bethlehemu na kuwaletea zawadi kwa sababu waliona nyota ya pekee iliyokuwa kwao alama ya kuzaliwa kwa mfalme mpya katika Uyahudi ikawaongoza hadi mjini Yerusalemu. Lakini walipompitia mfalme Herode Mkuu, huyo alikasirika akimwogopa mfalme mpya. Hata hivyo aliwaelekeza Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.

Yosefu alipata tena ujumbe kutoka kwa malaika akaondoka na mtoto na Maria kukimbilia Misri kabla ya askari wa Herode hawajaweza kumuua Yesu.

Baada ya kifo cha Herode walirudi kutoka Misri lakini hawakuenda tena Bethlehemu bali walihamia Nazareti katika mkoa wa Galilaya.

                                     

4.2. Habari za Krismasi katika Biblia Katika Injili ya Luka

Katika taarifa ya Luka mlango wa 1 na 2 Maria alipokea huko Nazareti ujumbe wa malaika mkuu Gabrieli kwamba atapata mimba halafu mtoto wa pekee.

Yosefu na Maria walikwenda Bethlehemu kwa sababu ya sensa iliyowataka kwenda katika mji asili wa ukoo wa Yosefu, mjukuu wa mfalme Daudi. Hapo Yesu alizaliwa katika hori la kulishia wanyama; wachungaji mabondeni walitangaziwa na malaika habari hiyo wakaja kumwona mtoto.

Baada ya kuzaliwa wazazi walimpeleka Yesu Yerusalemu katika hekalu kufuatana na sheria ya Agano la Kale Kitabu cha Kutoka 13.2; 13.15 halafu wakarudi kwao Nazareti.

                                     

5. Habari za Krismasi katika Korani

Korani pia ina habari za kuzaliwa kwake Yesu nabii Isa.

Sura ya tatu Al Imran, 42-47 ina habari za tangazo la malaika kwa Bikira Mariamu zinazofanana na Luka 1.

Sura ya 19 Mariamu, 16-34 inarudia tangazo la malaika kwa Mariamu na inasimulia kuzaliwa kwake Yesu chini ya mti wa mtende, halafu majadiliano kati ya Mariamu na ndugu zake. Mtoto mchanga Yesu akaanza kusema wakati wa kuzaliwa akimtetea mama yake dhidi ya ndugu zake.

                                     

6. Krismasi katika liturujia

Kama kawaida, imani na liturujia ya Kikristo zinaitikia haja za binadamu.

Mojawapo ni kukutana na watu wa kupendeza kwa wema wao.

Kipindi cha Noeli kinatimiza haja hiyo, kwa kuwa kinaadhimisha kuzaliwa kwa mtu mpya kabisa ambaye anatuvutia kwa wema wake na ambaye tukimuona tumemuona Mungu, tena tukimpokea tunazaliwa upya kama wana wa Mungu.

Leo amezaliwa kwa ajili yenu Mwokozi, ndiye Kristo Bwana”. Tunapoadhimisha Noeli tangazo hilo la malaika kwa wachungaji linatufikia sisi. Si kujidanganya, kana kwamba Yesu angezaliwa leo, wala hatukumbuki tu tukio la zamani, bali fumbo la kuzaliwa Bwana linatufikia leo katika liturujia na kutuletea neema zake. Hivyo tunaweza tukazaliwa upya kwa kushiriki kuzaliwa kwa kichwa chetu.

Liturujia inashangilia hivi," Lo! Mabadilishano ya ajabu! Mwana wa Mungu anakuwa mtu kusudi mtu awe mwana wa Mungu!”. Tena si binadamu tu, bali viumbe vyote vinapata heshima mpya kwa Neno wa milele kujifanya kiumbe.                                     

7. Desturi za Krismasi

Sherehe ya Krismasi imekuwa sikukuu muhimu sana katika tamaduni za mataifa yaliyoathiriwa na Ukristo. Kuna desturi nyingi zilizojitokeza katika karne zote za kusheherekea Krismasi. Sehemu ya desturi hizi zimeenea pia nje ya nchi za asili na hata kutumiwa na watu wasiofuata imani ya Kikristo.

 • Pango la Noeli lililoanzishwa na Fransisko wa Asizi mwaka 1223 kijijini Greccio Italia ya Kati na kuenea kila mahali kama sanaa inayoonyesha kwa njia mbalimbali jinsi Yesu alivyozaliwa.
 • Mapambo ya Krismasi: ni hasa nuru na taa za pekee. Alama za nyota kwa kukumbuka nyota iliyopeleka mamajusi hadi Bethlehemu inawekwa ndani na nje ya nyumba na maduka.
 • Mti wa Krismasi - ni ishara ya pekee ya Krismasi yenye asili katika Ujerumani kusini-magharibi ya karne ya 16 hivi. Asili yake iko katika maigizo yaliyosimulia hadithi za Biblia na mti wa Paradiso unaohusiana na masimulizi ya dhambi la kwanza na ujumbe wa Kristo kama mwokozi anayekuja kuondoa dhambi hilo. Kutoka maigizo ya kanisani ishara ya mti uliopambwa matunda uliingia katika nyumba za Wakristo ambako ulipambwa zaidi kwa matunda, keki tamu na pipi kwa watoto. Umekuwa mapambo ya nyumbani kwa majira ya Krismasi. Tangu Krismasi kuwa nafasi muhimu kwa uchumi kuna pia maduka mengi yanayoweka miti hii na katika mazingira ya kibiashara uhusiano wake na mti wa Paradiso umesahauliwa mara nyingi.
 • Zawadi za Krismasi - Martin Luther alitaka kuongeza umuhimu wa Krismasi kwa Wakristo ambao wakati wake walikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu. Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo. Hapo alirejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kufuatana na taarifa ya Injili ya Mathayo mlango 2. Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha kuwa nafasi muhimu ya biashara. Katika nchi nyingi mwezi Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine. Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na mapambo ya Krismasi katika maduka yanataka kuwahamasisha wateja kununua zawadi za majira.
 • Baba Krismasi
                                     
 • katika desturi za Krismasi za Marekani akifanana na masimulizi mengine katika tamaduni za Ulaya zinazojulikana kiasi kama Baba Krismasi kwa Kiswahili, jina
 • Mpya Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, siku hii ya nane baada ya Krismasi kwa kukumbuka tohara ya Yesu aliyofanyiwa siku hiyo, huadhimisha sherehe
 • lamaanisha mtoto kwa maana mtoto Yesu kwa sababu hutokea wakati wa Krismasi yaani sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu. Jina lilibuniwa na wavuvi wa Peru walioona
 • inayoadhimishwa na Kanisa la magharibi tarehe 24 Juni, miezi sita kabla ya Krismasi lakini ipo pia sikukuu ya kifodini chake. Kadiri ya Injili ya Luka, Yohane
 • kubariki nyumba, kula keki ya mamajusi watatu, kuogelea na kuondoa mapambo ya Krismasi Neno ἐπιφάνεια lilitumiwa na Wagiriki wa kale kumaanisha tendo ambalo
 • yaani 500 kwenye Visiwa vya Cocos Keeling na 560 kwenye Kisiwa cha Krismasi Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimalay ya Visiwa vya
 • aliyefika hapa 25 Desemba 1497. Aliita mahali Rio de Natal au mto wa Krismasi kutokana na tarehe ya kufika kwake. Hii ni chanzo cha jina Natal kwa
 • katika Vietnam Hanoi iliona uharibifu kutokana na mabomu ya Marekani. Krismasi ya 1872 tani 40, 000 za baruti zilitupwa Hanoi. Tangu muungano wa Vietnam
 • 8 Days of Christmas ni albamu ya Krismasi iliyoimbwa na Destiny s Child, na kutolewa na Columbia Records mnamo Oktoba 2001 ncini Marekani. Ilifika namba
 • sherehe ya Wamarekani weusi alioona ambao alitaka wawe na sikukuu tofauti na Krismasi aliyoona kama sikukuu ya Kizungu. Karenga alijitahidi kupamba sherehe ya
 • sherehe za ibada, kwanza katika kibanda cha muda lakini kwenye sikukuu ya Krismasi 1873 aliweka jiwe la msingi la kanisa. Steere alitumia mahali pa soko hilo

Users also searched:

...
...
...