Back

ⓘ Titanic
Titanic
                                     

ⓘ Titanic

Titanic ilikuwa meli kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast. Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani pamoja na mwenzake "Olympic".

Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki kati ya Uingereza na Marekani.

Kwenye safari yake ya kwanza iligongana na siwa barafu tar. 14 Aprili 1912 mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili.

Watu 2200 walikuwepo kwenye meli. Katika maji baridi takriban 1500 walikufa ni 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu.

Ajali ya Titani ilionyesha kasoro nyingi katika sheria kuhusu ujenzi wa meli na vifaa kama idadi maboti madogo ya dharura na sheria zilibadilishwa baadaye.

1997 filamu juu ya kuzama kwa Titanic ilitolewa ikapata sifa nyingi.

Users also searched:

...
...
...