Back

ⓘ Liberia
Liberia
                                     

ⓘ Liberia

Liberia yaani Nchi ya watu huru kwa Kilatini ni nchi iliyoko Afrika ya Magharibi. Imepakana na nchi za Ivory Coast, Guinea, na Sierra Leone.

Ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo hazikutawaliwa na Wazungu.

                                     

1. Historia

Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi 5%, mbali na machotara wa aina mbalimbali.

Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847.

Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani.

Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji.

Alama za taifa hili na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.

Liberia ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya miaka 1989-1996 na 1999-2003.

Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika nafasi ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson-Sirleaf.

                                     

2. Watu

Lugha rasmi ni Kiingereza, ambacho kinatumiwa na asilimia 15 za wakazi. Lugha za taifa ni 4: Kiingereza cha Kiliberia, Kikpelle, Kimeriko na Krioli.

Upande wa dini, wakazi kwa asilimia 85.5 ni Wakristo, hasa Waprotestanti, halafu Wakatoliki 5.8%. Waislamu ni 12.2%. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% tu.

                                     

3. Tazama pia

 • Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
 • Demografia ya Afrika
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
 • Orodha ya lugha za Liberia
 • Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
                                     

4. Viungo vya nje

 • Serikali ya Liberia

Liberia travel guide kutoka Wikisafiri

 • Liberia profile from the BBC News.
 • Liberia entry at The World Factbook
 • "Liberia Maps", Perry-Castañeda Library, University of Texas at Austin.
 • Chief of State and Cabinet Members
 • Liberia katika Open Directory Project
 • Wikimedia Atlas of Liberia
 • Liberia Archived Juni 7, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs.
                                     
 • Kikrumen - Tepo ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Cote d Ivoire na Liberia inayozungumzwa na Wakrumen. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kikrumen - Tepo nchini
 • wa Liberia ambaye anacheza kama beki wa klabu ya Barrack Young. Kamara alicheza kwa mara yake ya kwanza kimataifa katika timu ya taifa ya Liberia mwaka
 • ya Kiniger - Kongo nchini Liberia na Guinea inayozungumzwa na Wamann. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimann nchini Liberia imehesabiwa kuwa watu 188
 • Kiniger - Kongo nchini Liberia na Sierra Leone inayozungumzwa na Wagola. Mwaka wa 1991 idadi ya wasemaji wa Kigola nchini Liberia imehesabiwa kuwa watu
 • Kiniger - Kongo nchini Liberia na Sierra Leone inayozungumzwa na Waklao. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kiklao nchini Liberia imehesabiwa kuwa watu
 • Kimaninka - Konyanka ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Guinea na Liberia inayozungumzwa na Wamaninka. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kimaninka - Konyanka
 • wa timu ya taifa ya Liberia anayecheza kama kiungo. Allen anacheza katika klabu ya LISCR na anaiwakilisha timu ya taifa ya Liberia katika mashindano ya
 • Kiniger - Kongo nchini Liberia na Cote d Ivoire inayozungumzwa na Wakrahn. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kikrahn - Magharibi nchini Liberia imehesabiwa kuwa
 • Kimaninkakan - Mashariki ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia inayozungumzwa na Wamalinke. Mwaka wa 1986 idadi ya wasemaji wa Kimaninkakan - Mashariki
 • Kimende ni lugha ya Kiniger - Kongo nchini Sierra Leone na Liberia inayozungumzwa na Wamende. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kimende nchini Sierra Leone

Users also searched:

...
...
...