Back

ⓘ Lambo
Lambo
                                     

ⓘ Lambo

Lambo ni ukuta uliojengwa kwa kusudi la kuzuia mwendo wa maji au kubana maji katika eneo fulani. Mara nyingi malambo hujengwa kufunga njia ya maji ya mto. Lambo laweza pia kukusanya maji ya mvua kwenye njia ya mtelemko wake.

                                     

1. Shabaha ya kujenga lambo

Shabaha ya kujenga lambo ni hasa kupata akiba ya maji. Maji hutumiwa kwa ajili ya umwagiliaji, kama chanzo cha maji ya bomba kwa ajili ya watu au pia kwa utengenezaji wa umememaji.

Lambo hujengwa pia kwa shabaha ya kuzuia mafuriko.

Malambo hujengwa mara nyingi katika mabonde ambako milima ya pande zote mbili iko karibu na kupunguza mahitaji ya kujenga ukuta mkubwa mno.

Kuna pia malambo ya bahari ambayo yanajengwa kama hifadhi ya nyumba au mashamba dhidi ya maji ya bahari.

                                     

2. Shida za malambo

Kuna pia matatizo ya malambo:

 • Lambo linaweza kusababisha ajali na hata maafa likipasuka na kiasi kikubwa cha maji kilichozuiliwa na ukuta wake kushuka ghafla na kuharibu makazi ya watu, mashamba na miundombinu kwenye njia yake.
 • Ukuta unaathiri uwiano wa ekolojia; kwa mfano lambo la Aswan linazuia matope yenye rutuba yasifikie Misri
 • Mara nyingi wenyeji wamefukuzwa katika eneo la ziwa jipya bila kupewa makazi mazuri
 • Penye hatari ya tetemeko la ardhi uzani wa maji umeongeza matetemeko
 • Umwagiliaji katika nchi za joto unaweza kuharibu ardhi ukiiongezea chumvi kwa njia ya uvukizaji
                                     

3. Malambo makubwa ya Afrika

 • Lambo la Kariba kwenye mto Zambezi kati ya Zambia na Zimbabwe
 • Lambo la Cabora-Bassa Msumbiji.
 • Lambo la Aswan Ziwa la Nasser - Misri
 • Lambo la Akasombo Ziwa Volta - Ghana
 • Lambo la Kidatu Tanzania
 • Lambo la Mtera Tanzania

Users also searched:

...
...
...