Back

ⓘ Bahari ya Aktiki
Bahari ya Aktiki
                                     

ⓘ Bahari ya Aktiki

Bahari ya Aktiki ni bahari inayozunkguka ncha ya kaskazini. Ni sehemu ya eneo la Aktiki. Wataalamu wengine huitazama kama bahari ya pekee lakini wengine huona ni bahari ya pembeni ya Atlantiki. Kina kikubwa kiko karibu na visiwa vya Spitzbergen chenye mita 5.608.

Bahari ya Aktiki iko kati ya pwani za Asia ya Kaskazini, Alaska na Kanada katika Amerika ya Kaskazini, Greenland na Skandinavia Ulaya. Eneo lake ni 14.056 km². Kati ya Greenland na Skandinavia kuna uwazi kubwa unaojifungua kwa Atlantiki ya Kaskazini na mlango wa Bering unaunganisha bahari hii na Pasifiki.

Sehemu kubwa ya eneo lake hufunikwa na barafu yenye unene wa mita 3 lakini sehemu hii imeanza kupungua kutokana na kupanda kwa halijoto duniani.

Mito muhimu inayoingia ni Ob, Yenissei, Lena na Kolyma upande wa Siberia Urusi halafu mito ya Yukon na Mackenzie upande wa Amerika ya Kaskazini.

                                     

1. Bahari za pembeni

 • Bahari ya Lincoln
 • Bahari ya Norwei
 • Bahari ya Mashariki ya Siberia
 • Bahari ya Greenland
 • Bahari ya Barents
 • Bahari ya Kara
 • Bahari ya Baffin
 • Bahari ya Laptev
 • Bahari ya Chukchi
 • Bahari ya Beaufort
 • Bahari Nyeupe

Users also searched:

...
...
...