Back

ⓘ Mfereji wa Mariana
Mfereji wa Mariana
                                     

ⓘ Mfereji wa Mariana

Mfereji wa Mariana ni sehemu ya chini kabisa kwenye uso wa dunia yetu. Ni mfereji wa Bahari ya Pasifiki ambako kina cha maji hufikia mita 10.293 kutoka uso wa bahari hadi sakafu yake. Mifereji kwenye misingi ya bahari hulinganishwa pia na mabonde makali au korongo chini ya maji.

Mfereji huu uko kando ya Visiwa vya Mariana karibu na Guam. Ni mahali ambako bamba la Pasifiki hujisukuma chini ya Bamba la Ufilipino.

Sehemu ya chini kabisa ilifikiwa katika historia mara mbili na nyambizi za kisayansi. Mara ya kwanza ilikuwa safari ya chombo cha Trieste cha mchunguzi wa bahari Auguste Piccard tar. 23 Januari 1960 na 1995 Kaiko kutoka Japani.

Users also searched:

...
...
...