Back

ⓘ Waetruski
Waetruski
                                     

ⓘ Waetruski

Waetruski walikuwa taifa maalumu katika Italia ya kale. Waliishi katika Italia ya Kati na kuanzisha mji wa Roma.

Mwanzo wa ustaarabu wao ulikuwa mnamo mwaka 800 KK ukaishia katika miaka ya mwisho ya Jamhuri ya Roma.

Waliacha mabaki ya utamaduni wenye mifano bora ya uchoraji na ujenzi. Utamaduni wao ulipotea katika mazingira ya Kiroma.

                                     

1. Historia

Wataalamu wengine huamini kuwa walihamia Italia kutoka Anatolia, lakini utafiti wa hivi karibuni umethibitisha kuwa ni wenyeji wa Italia, si tofauti sana na Walatini. Inawezekana walifikiriwa kutokea Mashariki kwa sababu tu waliathiriwa sana na ustaarabu wa Wagiriki.

Mwandiko wao uliotunzwa ukutani mwa makaburi wasomeka kirahisi kwa sababu ulifuata alfabeti ya Kigiriki pamoja na athira ya Wafinisia wa Mediteranea ya magharibi. Hata hivyo lugha ya Kietruski si rahisi kuielewa kwa sababu msamiati ni wa pekee; hadi sasa ni takriban maneno 200 tu yanayoeleweka.

Waetruski walianzisha miji 12 waliohusiana kama shirikisho. Inaaminika ya kwamba misingi ya mji wa Roma ni ya Kietruski pia. Wafalme wa kwanza wa Roma walikuwa wa asili ya Kietruski. Hivyo hadi mwaka 396 Roma ilikuwa chini ya athira ya Waetruski.

Mwaka ule jeshi la Roma likateka na kuangamiza mji wa Veiji na kumaliza kipaumbele ya Waetruski katika Italia. Miji kadhaa ya Kietruski ilifanya mikataba ya Roma ikapewa uraia wa Kiroma hadi mwaka 90 KK. Baadaye utamaduni wa Kietruski ulianza kupotea wakati watu walipoacha kutumia lugha yao.

Users also searched:

...