Back

ⓘ Ustaarabu wa Indus
Ustaarabu wa Indus
                                     

ⓘ Ustaarabu wa Indus

Ustaarabu wa Indus ulikuwa ustaarabu wa Zama za Shaba uliopatikana katika bonde la mto Indus katika Pakistan na Uhindi ya leo.

                                     

1. Ugunduzi

Habari zake zimepatikana kwa njia ya uvumbuzi wa kiakiolojia kuanzia miaka ya 1880.

Mji wa kwanza kugunduliwa ulikuwa Harappa iliyoangaliwa na Mwingereza Masson aliyedhani ni mmoja wa miji iliyotembelewa na Aleksanda Mkuu; utafiti wa baadaye ulionyesha umri wake ni wa kale zaidi. Mwanaakiolojia Mhindi R. D. Banerji alitambua mnamo 1923 kwamba mabaki ya Harappa yalifanana na yale ya Mohenjo-daro iliyopo kilomita 600 upande wa kusini. Baada ya kugunduliwa kwa sehemu nyingine yenye maghofu ilionekana kwamba hayo ni mabaki ya ustaarabu ulioanza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea katika bonde la mto Indus pamoja na matawimito yake makubwa. Pamoja na miji mingi midogo mabaki ya miji mikubwa mitano yamegunduliwa ambayo ni Harappa, Mohenjo-daro na Ganeriwala katika Pakistan ya leo na Dholavira na Rakhigarhi upande wa Uhindi ya leo.

                                     

2. Miji yake

Ustaarabu huo ulianza wakati wa Zama za Shaba ukaendelea kustawi hadi takriban mwaka 1500 KK. Kwa hiyo ilidumu muda mrefu sana.

Watu wa Bonde la Indus walikuwa wajenzi hodari. Miji yao ilipangwa vizuri. Ilikuwa na mfumo wa majitaka, kwa kuweka mfereji wa majitaka kando ya kila mtaa. Hakuna mifano mingine wa miundombinu hiyo katika sehemu nyingine za Dunia kwa wakati ule. Nyumba zilikuwa na ghorofa moja au mbili, na nyingi zilikuwa na chumba cha bafu lakini kulikuwa pia na bafu za umma. Maji yalipelekwa mjini na kugawiwa kwa matangi ya nyumba. Nyumba zilikuwa pia na choo, na uchafu wa nyumba jirani ulipitishwa kwa kumwaga maji katika mabomba ya kitofali hadi shimo kubwa; mashimo hayo yalisafishwa baada ya muda, labda kwa kutumia yaliyomo kama samadi mashambani.

Tofauti na tamaduni nyingine za milenia ya tatu na ya pili KK katika Misri ya Kale na Mesopotamia hawakuacha majengo makubwa kama mahekalu au majumba ya kifalme. Majengo makubwa zaidi yaliyoweza kutambuliwa yanaonekana kuwa ghala za nafaka.

                                     

2.1. Miji yake Maandishi

Watu walitumia aina ya maandishi lakini hadi leo haijawezekana kuyasoma. Kwa hiyo haijulikani walitumia lugha gani. Mwandiko ulitumia takribani alama 400 na mifano mingi inaonekana kama mabaki ya mihuri iliyoonyesha asili ya bidhaa fulani au yaliyomo ya chombo. Maandishi yote ni mafupi sana yenye alama chache tu.

                                     

2.2. Miji yake Mwisho

Haijulikani ni nini kilichosababisha mwisho wa ustaarabu huo. Tangu mwaka 2000 KK kuna dalili za kushuka kwa hali ya uchumi. Mnamo mwaka 1700 KK miji mingi haikukaliwa tena. Utafiti wa masalia ya binadamu kutoka makaburi ya siku zile unaonyesha kuongezeka kwa majeruhi na dalili ya magonjwa kama ukoma na kifua kikuu. Wengine walifikiri ilikuwa labda uhamiaji wa makabila ya Kihindi-Kiulaya walioanza kuingia Uhindi mwisho wa milenia ya pili. Wengine wanaona ilikuwa mabadiliko ya tabianchi hasa kipindi kirefu cha ukame, pamoja na mfululizo wa matetemeko ya ardhi.

                                     

3. Viungo vya Nje

Mohenjo-daro travel guide kutoka Wikisafiri

  • An invitation to the Indus Civilization Tokyo Metropolitan Museum
  • Cache of Seal Impressions Discovered in Western India
  • Harappa and Indus Valley Civilization at harappa.com

Users also searched:

nadharia ya usasa na usasa leo,

...
...
...