Back

ⓘ Jordan Riber
                                     

ⓘ Jordan Riber

Riber alizaliwa katika familia ya son John na Louise Riber ambao wote ni wanafamilia katika mambo ya filamu; alikulia katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare na muda mwingi aliutumia katika kujifunza masuala ya utengenezaji wa filamu. Mwaka 2004 alimaliza masomo yake katika chuo cha Fairhaven College, nchini Marekani alikosomea mambo ya utayarishaji wa filamu.

                                     

1. Taaluma

Mwaka 2012, aliongoza tamthilia ya Siri ya Mtungi, ilIYokuwa na nyota kama Cathryn Credo, Beatrice Taisamo, Yvonne Cherrie na wengine. tamthilia ambayo ilichaguliwa kama tamthilia bora katika tuzo za 2014 Africa Magic Viewers Choice Awards AMVCA.

Mwaka 2017 aliongoza filamu ya Hadithi za Kumekucha: Tunu.

Mwaka 2018 aliongoza filamu nyingine ya Hadithi za Kumekucha:Fatuma aliyoitarisha na kuihariri yeye mwenyewe, ambao nyota wake walikuwa ni Cathryn Credo,Beatrice Taisamo na Ayoub Bombwe. Mwaka huohuo alitayarisha na kuongoza filamu ya Bahasha, iliyochezwa na Ayoub Bombwe, Godliver Gordian, Omary Mrisho na Cathryn Credo.

Users also searched:

...