Back

ⓘ Anna Line
Anna Line
                                     

ⓘ Anna Line

Anna Line alikuwa mwanamke Mwingereza aliyebadilisha imani yake ya dini kutoka Ushirika wa Anglikana kuingia Kanisa Katoliki.

Kwa vile aliwaficha mapadri nyumbani mwake na kuhudhuria Misa ya Kikatoliki, alipelekwa mahakamani na kuuawa.

Mwaka 1929 alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenyeheri na mwaka 1970 alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 27 Februari.