Back

ⓘ Baldomero wa Lyon
                                     

ⓘ Baldomero wa Lyon

Baldomero wa Lyon alikuwa mhunzi wa mji huo, leo nchini Ufaransa, ambaye alijulikana kwa maadili na ukarimu wake.

Miaka yake ya mwisho alimfuata abati Vivensioli kwenda kuishi na wamonaki na alipewa daraja ya shemasi mdogo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Februari.