Back

ⓘ 2 Pallas
2 Pallas
                                     

ⓘ 2 Pallas

2 Pallas ni asteroidi ya pili iliyowahi kutambuliwa katika Mfumo wa Jua. Iligunduliwa na mtibabu na mwanaastronomia Mjerumani Heinrich Wilhelm Matthäus Olbers mnamo 28 Machi 1802.

Jina la "2 Pallas" inaunganisha jina lililotolewa na Olbers, pamoja na namba ya asteroidi iliyojulikana. Jina lenyewe limanrejelea Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu katika dini ya Ugirki ya Kale.

2 Pallas ina masi inayokadiriwa kuwa asilimia 7% ya masi yaote ya ukanda wa asteroidi. Ni asteroidi kubwa ya tatu kulingana na masi yake, na ya pili kwa kuangalia kipenyo chake. Umbo lake linafanana na duaradufu yenye vipenyo kati ya km 500 na km 582.

Users also searched:

...
...
...