Back

ⓘ Antonino wa Sorrento
Antonino wa Sorrento
                                     

ⓘ Antonino wa Sorrento

Antonino wa Sorrento alikuwa kwanza mmonaki Mbenedikto huko Monte Cassino.

Monasteri yake ilipovamiwa na Walombardi, hakukimbilia Roma kama wenzake, bali alikwenda kuishi kama mkaapweke karibu na Sorrento kwenye pwani ya Mediteranea nchini Italia.

Mwishowe akawa abati wa monasteri ya jirani.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Februari.