Back

ⓘ Ansberto wa Rouen
Ansberto wa Rouen
                                     

ⓘ Ansberto wa Rouen

Ansberto wa Rouen alikuwa askofu wa Rouen miaka 683 - 690.

Baada ya kushika vyeo vikubwa katika ikulu alijiunga na Wabenedikto na miaka sita baadaye akawa abati. Hatimaye alifanywa askofu hadi alipoondolewa na kurudia maisha ya monasterini.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Februari.