Back

ⓘ Alphonse Menyo
                                     

ⓘ Alphonse Menyo

Alizaliwa Accra, Ghana. Baba yake, Bernard Menyo, alitokea Afrika Mashariki na aliwahi kuwa mwanafunzi wa National Film and Television Institute NAFTI. Bernard alishinda tuzo kwenye Panafrican Film and Television Festival of Ouagadougou FESPACO kutokana na filamu ya Whose fault. Mama yake Menyo, Eugenia, ametokea Ghana ana fanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali.

                                     

1. Kazi

Menyo alihudhuria akademi ya uigizaji filamu ya Ghallywood Accra kusomea sinema na maigizo. Alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2009 kwa kuigiza jukwaani. Mwaka 2015 alikuwa muhusika katika filamu ya Freetown kuhusu uhuru wa Marekani, iliyoongozwa na Garret Batty. Filamu hiyo ilionyeshwa mara kadhaa katika matamasha ya kimataifa ya filamu na iliteuliwa mara kadhaa katika tuzo za filamu za Ghana.

Menyo aliigiza filamu yake ya kwanza ikijulikana kama Utopia. Filamu hiyo ilipata teuzi nne katika tuzo za filamu za Ghana. Mwaka 2017, Utopia ilikua filamu pekee ya Ghana iliyochaguliwa kuonyeshwa katika maonyesho ya filamu ya Helsinki HAFF.

Users also searched:

...