Back

ⓘ Tamy Moyo
                                     

ⓘ Tamy Moyo

Thamsanqa Tamy Moyo ni mwigizaji wa kike na mwimbaji wa Zimbabwe. Anajulikana Sana kwa wimbo wake wa Ndibereke aliyeimba mwaka 2016, mwaka 2020 Alipata jukumu la kuigiza katika filamu ya Gonarezhou.

                                     

1. Maisha binafsi

Baba yake, Richard Kohola ni mtangazaji wa Star FM Zimbabwe maarufu kwa jina la ’RK The Music Doctor’’. Alilelewa na mama yake Doris Moyo Pamoja na babu yake Makwara.

                                     

2. Kazi

Akiwa na miaka 7 pekee, alianza kuimba katika kwaya ya watu wazima. Alihitimu elimu yake ya msingi kutoka shule ya Lusitania na baadae kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Westridge High School. Alipofika kidato cha kwanza, wakati huo akiwa na miaka 13, alijiunga na wanamuzuki mashuhuri kama Joe Thomas, Oliver Mtukudzi, Stunner, Ba Shupi, na Alexio Kawara. Baadaye akawa balozi wa Watoto nchini Zimbabwe, na kufanikiwa kuwa balozi mdogo zaidi katika historia ya Zimbabwe. Mwaka 2008, Tamy aliunda kikundi cha kwaya kwa jina la Uganda African Choir, akiwa na wengine watatu, hii ilikua huko Madison Square, New York wakati wa shughuli ya kihisani.

Aliandika na kuimba wimbo kwa jina la, Cry For Help, wimbo huo ulihamasisha Watoto kupiga simu za kuomba msaada wakiwa na shida kwenda namba 116 bure. Mnamo mwaka 2012, kwa mara ya kwanza Tamy aliachia albamu yake ya kwa jina la Celebrate Yo Lyf. hii ilimfanya apate nafasi ya kutumbuiza katika matamasha makubwa ya muziki nchini Zimbabwe kama ’Harare International Festival of the Arts’’ na Shoko Festival. Pia alishiriki katika sherehe za tuzo za ’National Arts Merit Awards’’ na mashindano ya ulimbende ya ’Miss Tourism Zimbabwe’’ ambamo alitumbuiza mwezi Novemba mwaka 2016.

Mwaka 2017, Tamy alialikwa na mtayarisha wa filamu Sydney Taivavashe kuwa mhusika katika filamu ya Gonarezhou. Filamu hyo ilitengenezwa kwa ushirikiano na Shirika la wanyamapori na uhifadhi wa Wanyama la nchini Zimbabwe. In the film Tamy played the role Chipo as his debut cinema appearance. In the same year, she had her first nomination in the National Arts Merit Awards NAMA awards for the excellence in her role.

Mwaka 2019, Tamy aliteuliwa katika kinyang’anyiro cha msanii bora wa kike nyanda za Afrika ya Kusini karika tuzo za AFRIMA zilizofanyika nchini Ghana.