Back

ⓘ Sibongile Mlambo
                                     

ⓘ Sibongile Mlambo

Sibongile Mlambo ni mwigizaji wa Zimbabwe anayefanya shughuli zake nchini Marekani. Anafahamika kwa kuwa mhusika mkuu katika filamu za mwendelezo za tovuti ya Netflix ambazo ni Lost in Space, filamu ya mwendelezo ya the Starz historical adventure television, Black Sails, Honey 3: Dare to Dance na The Last Face. Pia anafahamika kwa uhusika wake kama Tamora Monroe katika filamu ya mwendelezo ya Teen Wolf, Donna katika filamu ya mwendelezo ya Freeform, Melusi katika mchezo wa Ubisoft.

                                     

1. Maisha ya awali

Mlambo alizaliwa Zimbabwe na baba yake ni daktari. Mlambo ana dada ambaye pia ni mwigizaji. Mlambo aliondoka Zimbabwe mwaka 2005 kuelekea nchini Marekani kwaajili ya masomo yake. Ameishi Texas, New York na Hispania. Mwaka 2011 Mlambo alikuwa akiishi Afrika ya kusini na kufanya kazi zake Cape Town na Johannesburg. Mlambo later moved back to the United States, settling in Los Angeles. Mlambo alisoma kifaransa na kihispania katika chuo kikuu cha Methodist.

                                     

2. Mitindo

Mlambo alikuwa mwana mitindo katika kampeni ya Nivea barani Afrika. Mwaka 2007 Mlambo alikuwa mshindi wa pili katika shindano la walimbwende wa zim-USA.

Uigizaji

Ameigiza kama mhusika mkuu katika filamu ya Black Sails, Honey 3: Dare to Dance na Footloose. Pia alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya The Last Face aliyeigiza kama Assatu na alikuwa dada yake Chadwick Boseman katika filamu ya Message From The King.