Back

ⓘ Quasi Blay Jr.
                                     

ⓘ Quasi Blay Jr.

Quasi Blay Jr. ni mwigizaji kutoka nchi ya Ghana. Anajulikana sana kwa majukumu yake katika filamu ya "Adoma" na "Grilled". Ameonyeshwa katika sinema kumi na tano na safu nne za runinga.

                                     

1. Maisha ya awali

Alizaliwa nchini Ghana akiwa mtoto wa tatu katika familia yenye ndugu watano, wanaume wanne na wa kike mmoja. Alimaliza elimu ya juu na ya chini katika shule ya Great Lamptey Mills, Kisha akaendelea na masomo yake ya Sekondari katika Shule ya Aburi SHS. Alichukua elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Koforidua na kupata Stashahada ya Juu ya Kitaifa ya Ununuzi na Usambazaji wa bidhaa.

                                     

2. Kazi

Alianza kazi ya uigizaji mnamo mwaka 2016 kama mtoto, akionekana katika filamu ya "Grey Vust", "Grilled", na safu ya "Deju Vu".Alipokea tuzo ya heshima kama mwigizaji bora wa Kiume katika tuzo ya Social Media Entertainment.Baadaye aliteuliwa kama Mwigizaji Bora katika jukumu lake la kuongoza katika Toleo la 9 la Tuzo za Sinema za nchini Ghana katika filamu ya "Adoma".