Back

ⓘ Carole Gray
                                     

ⓘ Carole Gray

Carole Gray alikuwa mcheza dansi na mwigizaji wa filamu na maonyesho ya jukwaani ambaye katika kazi yake hapo awali alianzia nchini Uingereza na alijulikana sana kwa uhusika wake katika muziki wa jumba la Sanaa la West End miaka ya 1960.

Alizaliwa Rhodesia Kusini, akafika nchini Uingereza mwaka 1956, na kuanza kazi yake ya uigizaji kwa miaka 12, alionekana katika filamu mbalimbali mojawapo iliyompatia umaarufu ni filamu ya The Avengers, lakini filamu iliyomtambulisha ni ya mchumba wake Cliff Richard, bibie Toni kwa jina la The Young Ones ya mwaka 1961.

Baada ya hapo, alijitokeza katika filamu nyingine tofauti hususani filamu za kutisha kama vile, Curse of the Fly, Devils of Darkness, na Island of Terror, na alipewa jina la utani la "Scream Queen". Mnamo mwaka 1968, alirudi nyumbani Afrika ambapo alishiriki katika maonyesho ya jukwaani kama Harvey", mwaka 1968, Fiddler on the Roof, mwaka 1969, na maonyesho ya Taubie Kushlick ya ’No, No, Nanette’’ katika ukumbi wa Alexander Theatre, Johannesburg, mwaka 1972.

                                     

1. Maisha binafsi

Carole aliolewa na mume wake wa kwanza Graham Du Toit, mnamo Disemba 1957. Walipotalakiana, ndoa yake ya pili ilikuwa na Douglas Cullinan, mfanyabiashara wa almasi.

                                     

2. Sehemu ya Sanaa

  • The Brides of Fu Manchu 1966 - Michel Merlin
  • Curse of the Fly 1965 - Patricia Stanley
  • Island of Terror 1966 - Toni Merrill
  • Rattle of a Simple Man 1964 – Nesi wa hospitali ya wilaya
  • Duel at Sundown 1965 - Nancy Greenwood
  • The Prince and the Showgirl 1957 – Mcheza densi
  • Oh! What a Lovely War 1969 – muimbaji wa kiitikio
  • Devils of Darkness 1965 - Tania
  • The Young Ones 1961 - Toni

Users also searched:

...