Back

ⓘ Anisi wa Thesalonike
                                     

ⓘ Anisi wa Thesalonike

Anisi wa Thesalonike alikuwa askofu wa mji huo kaskazini mwa Ugiriki kuanzia mwaka 383.

Alitetea imani sahihi kuhusu umungu wa Yesu Kristo na ubikira wa kudumu wa Bikira Maria.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Desemba.