Back

ⓘ Antoni wa Lerins
Antoni wa Lerins
                                     

ⓘ Antoni wa Lerins

Antoni wa Lerins alikuwa mmonaki maarufu kwa utakatifu na miujiza yake.

Baada ya kulelewa na Severino wa Noriko, alipofikia umri wa miaka 20 alijiunga na monasteri huko Ujerumani, halafu akawa mkaapweke katika Italia Kaskazini. Kwa kuwa alizidi kupata wafuasi na heshima, miaka miwili kabla hajafa alihamia Lerins ili kupata faragha aliyoitamani.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 28 Desemba.