Back

ⓘ Aleksanda Briant
Aleksanda Briant
                                     

ⓘ Aleksanda Briant

Aleksanda Briant, S.J. alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uingereza.

Baada ya kuacha ushirika wa Anglikana ili kujiunga na Kanisa Katoliki, alipata upadrisho huko Ufaransa mwaka 1578 akatumwa kwao alipofanya utume miaka 3. Alipokuwa gerezani alijiunga na Wajesuiti na hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius IX mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Desemba.