Back

ⓘ Segun Arinze
                                     

ⓘ Segun Arinze

Segun alizaliwa Onitsha, jimbo la Anambra na baba wa kabila la Yoruba na mama wa kabila la Igbo. Ni mzaliwa wa Badagry, jimbo la Lagos. Alihudhuria Victory College of Commerce huko Ilorin, kisha akaenda Taba Commercial College iliyopo jimbo la Kaduna baada ya kumaliza elimu yake ya shule ya upili.

Alisomea Michezo ya Kuigiza katika Obafemi Awolowo University. Anafahamika almaarufu kama Black Arrow ambapo alipata jina hilo katika uhusika alioigiza.

Alimuoa mwigizaji mwenzake wa Nollywood Anne Njemanze, ambae baadaye alikuja kuwa na maisha ya ndoa mafupi kuliko alioyaishi. Wanandoa hao walikua na binti mmoja, Renny Morenike, aliyezaliwa tarehe 10 Mei.

                                     

1. Kazi

Alianza uigizaji ndani ya Ilorin. Mbali na uigizaji, Segun pia ni mkufunzi wa waigizaji na kwa sasa anafanya kazi na African international film festival kwa kutoa maarifa kwa kizazi kijacho cha waigizaji.

                                     

2. Filamu zilizochaguliwa

 • Deepest Cut 2018 - with Majid Michel and Zach Orji
 • Gold Statue 2019
 • To Love a Thief
 • Across the Niger
 • An eye for an eye
 • A Place in the Stars 2014
 • Fragile Pain
 • Women in Love
 • Church Business
 • Family on Fire 2011
 • Chronicles with Onyeka Onwenu and Victor Osuagwu
 • Darkest Night
 • Anini
 • Invasion 1897 2014
 • The Island Movie 2018
 • Silent Night
 • Extra Time
 • 30 Days