Back

ⓘ Uche Elendu
                                     

ⓘ Uche Elendu

Uche Elendu ni mwigizaji na mwimbaji wa kike kutoka nchini Nigeria na pia ni mjasiriamali. Alifafanuliwa kama mmojawapo wa waigizaji wenye sura thabiti katika tasnia ya sinema ya Nigeria. KutokEa kwake kwa mara ya kwanza ni mnamo mwaka 2001. Mwaka 2010 alichukua mapumziko kutoka tasnia ya burudani ya Nigeria. Kulingana na machapisho ya Vanguard, Elendu ameshiriki zaidi ya sinema 200 za kinigeria.

                                     

1. Maisha ya awali

Elendu alizaliwa katika jimbo la Abia kusini mashariki mwa Nigeria, ambapo ni makazi ya watu wa kabila la Igbo. Elendu ni mzaliwa wa kwanza katika familia yao ana wadogo zake watatu wote wa kiume. Baba yake ni mstaafu wa serikali pia mjasiriamali na mama yake ni mwalimu.Elendu alihitimu chuo kikuu cha Imo State University na kupata shahada ya uhusiano wa kimataifa.

                                     

2. Kazi

Elendu alijiunga rasmi na tasnia ya filamu ya nchini Nigeria mwaka 2001. Alianza kazi yake ya uigizaji kwa kushiriki katika filamu inayofahamika kwa jina la Fear of the Unknown.Elendu kutokana na ndoa alichukua mapumziko marefu katika uigizaji ambapo hatua hii ilimharibia kazi yake ya kuigiza. Mwaka 2015 alirudi katika kazi ya uigizajina kua mshiriki mkuu katika filamu inayo famika kwa jina la Ada Mbano. Filamu hii ilikua kichocheo katika kazi yake.

Katika moja ya mahojiano na The Sun ya nchini Nigeria, Elendu alielezea tabu alizopata kurudi katika tasinia ya uigizaji baada ya kuchukua likizo ya mda mrefu. Alielezea uhusika wake katika filamu ya Ada Mbano na jinsi ilivyokua na mchango chanya katika kazi yake. Wakati wa mahojiano, alielezea kwa ufupi mchango wa filamu hiyo kwa kusema" Filamu iliyonirudisha mimi ni ya Ada Mbano ”.

                                     

3. Maisha binafsi

Elendu, japokuwa kwa sasa ana talaka, aliolewa mwaka 2012 na bwana Ogochukwu Igweanyimba mjini Owerri, Imo, na kupata watoto wawili wa kike. Elendu alipata ajali ya barabarani ambapo mojawapo ilimfanya apoteze fahamu.

                                     

4. Filamu zilizochaguliwa

 • Twilight SIsters 2009
 • Bottom Of My Heart 2008
 • Missing Rib 2007
 • Yankee Girls 2008
 • Omaliko 2005
 • Old Testament 2007
 • Chicken Madness 2006
 • Holy Cross 2006
 • Occultic Battle 2005
 • Beyond The Verdict 2007
 • Mountains Of Evil 2007
 • Before Ordination 2007
 • Most Wanted Bachelor 2007
 • Don’t Wanna Be A Player 2008
 • Woman On Top 2005
 • To Love And Live Again 2005
 • Brain Wash 2007
 • Nigerian Girls 2009
 • Johnbull & Rosekate 2007
 • Return Of The Ghost 2006
 • Angelic Bride 2008
 • Give It Up 2008
 • Security Risk 2005
 • The Rain Makers 2009
 • Lost In The Jungle 2007