Back

ⓘ Michael Kasaija
                                     

ⓘ Michael Kasaija

Michael Kasaija ni mwigizaji, mwanamitindo, mtengeneza dansi na mnenguaji kutoka Uganda.Aliigiza kwa mara ya kwanza kama muigizaji mkuu kwenye filamu ya Bala Sese ya mwaka 2015 akiwa na mchumba wake wa wakati huo Natasha Sinayobye.

                                     

1. Maisha ya Mwanzo

Michael alilelewa Kampala Uganda na alisoma Busoga College Mwiri na Caltec Academy.Akiwa Chuo kikuu cha Makerere, Michael alipata shahada ya usimamizi wa biashara na kushiriki katika mashindano na matamasha ya unenguaji na dansi.

                                     

2. Kazi

Steve Jean alimuajiri Michael baada ya shule kuwa mnenguaji wake mkuu, kitu kilichomfikisha Michael kwa Pamela Basasirwaki, ambaye alianzisha nae mahusiano. Kama mwanachama wa kundi la dansi la Obsessions, Pamela alimtambulisha Michael kwenye kundi na alikubalika mara moja. Alikuja mnenguaji mwingine katika kundi, Natasha Sinayobye ambaye hakumhitaji tena na wawili hao waliondoka kwenye kundi 2005 na kuanzisha kundi lao la KOMBAT Entertainment Ltd. Chini ya Kombat alifanikiwa kupata onyesho lake kubwa akitumbuiza katika sherehe za wakuu wa Nchi za CHOGM 52 zilizofanyika Uganda mwaka 2007. Hivi karibuni Michael alijipatia kazi kama meneja wa makundi machanga ya maigizo kwenye majaribio ya maonyesho, katika kipande cha tisa cha mfululizo wa maigizo ya usiku wa mahaba ya kundi.Alikuwa pia mmoja wa majaji kwenye tamasha la NTVs Xp sambamba na wanamuziki, Isiah Katumwa, Jackie Chandiru na Bebe Cool.

Users also searched:

...