Back

ⓘ Nana Gichuru
                                     

ⓘ Nana Gichuru

Ephex Kanana Gichuru alikuwa mwigizaji na muendesha vipindi vya televisheni nchini Kenya.

Kama muigizaji, alijulikana kwa uhusika wake katika maonyesho ya televisheni kwa majina ya Noose of Gold, Demigods na How to Find a Husband. Kama mtangazaji, alitakiwa aelezee kipindi cha Interior Designs, maonyesho ya uhalisia ya ki Kenya, kabla ya kifo chake. Pia alikuwa ni miongoni mwa wafanyakazi katika shirika la ndege la nchini kenya. Aliolewa na Richard Wainaina.

                                     

1. Kazi

Gichuru alianza kuzalisha filamu kama Noose of Gold mwaka 2010 na Demigods mwaka 2011. Kazi zake za hivi karibuni katika Uchekeshaji ni How to Find a Husband na onyesho la ukweli Interior Designs

                                     

2. Kifo

Takriban majira ya saa 4 asubuhi, 22 Septemba mwaka 2015, Nana alikua akisafiri ndani ya gari lake aina ya BMW, alipofika makutano ya barabara ya Utawala, aligonga lori na kufa papo hapo. Alikufa akiwa na miaka 28. Kifo chake kilitokea siku kumi baada ya yeye mwenyewe kujitabiria kifo kupitia kurasa zake za kijamii. Ibada ya kumbukumbu ya kifo chake ilifanyika tarehe 30 Septemba 2015 katika kanisa la Ruaraka Methodist Church. Alizikwa tarehe 2 Oktoba 2015 nyumbani kwao Kaaga, Meru.

Users also searched:

...